Mkurugenzi AICC afariki dunia

Mkurugenzi AICC afariki dunia

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AlCC),   Elishilia Kaaya amefariki dunia jana Ijumaa Julai 9, 2021.

Arusha. Mkurugenzi wa kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AlCC),   Elishilia Kaaya amefariki dunia jana Ijumaa Julai 9, 2021.

Kaaya  amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa ndani ya CCM Mkoa wa  Arusha ikiwemo mjumbe wa kamati ya siasa mkoa.

Amekutwa na umauti  katika hospital ya AICC inayomiliki kituo cha AICC.

Kaimu mkurugenzi mwendeshaji wa kituo hicho,   Mkude Mushi amesema upo nyumbani kwa marehemu  kijiji cha Nguruma  wilayani Arumeru..

Mkuu wa Mkoa Arusha,  John Mongela ametoa wito kwa wakazi Arusha kuchukua tahadhari dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa corona.

Mongela ameagiza wakuu wa wilaya kusimamia tahadhari zote dhidi ya ugonjwa huo.

Kifo cha Kaaya kimetokea siku mbili baada ya vifo vya watu kadhaa akiwemo  mchungaji Dk Leonard Dafa na mkewe.