Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkurugenzi Gairo akamatwa na polisi tuhuma wizi wa mabati

Mkurugenzi Gairo adakwa na polisi tuhuma wizi wa mabati

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale anashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,100 mali ya halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.


Morogoro. Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale anashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,100 mali ya halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,   Fotunatus Muslimu amesema hayo leo Jumanne  Agosti 24, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Muslimu amesema kutokana na wizi huo watu wengine saba wanashikiliwa na wanadaiwa kushirikiana  mkurugenzi huyo na wanaendelea kuhojiwa.

Awali Mwambambale alikuwa mkurugenzi wa halmamshari ya Kilosa kabla ya kuhamishwa halmashauri ya Gairo.

Wizi wa mabati hayo  ulifanyika Juni 17, 2021 eneo ya ujenzi kitongoji cha Mvumi B  wilayani Kilosa  katika stoo ya halmashauri hiyo ambayo haikuvinjwa ambapo stoo hiyo haikuvunjwa.