Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmiliki wa Peacock Hotel afariki dunia

Mmiliki wa Peacock Hotel afariki dunia

Muktasari:

  • Mmiliki wa hotel ya Peacock hotel, Joseph Mfugale amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mmiliki wa hoteli ya Peacock, Joseph Mfugale amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa ndugu za Mfugale aliyetajwa kuwa msemaji wa familia, Expedito Mfugale alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema hawezi kuzungumzia.


Hata hivyo, mmoja wa ndugu zake ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini kwa kuwa si msemaji wa familia, anasema Mfugale amefariki le Julai 31 asubuhi na msiba uko nyumbani kwake Kibamba Dar es Salaam.


“Ni kweli kaka amefariki leo asubuhi. Alikuwa anaumwa, muda mrefu, lakini swali kwamba alikuwa anaumwa nini ni la kifamilia,” alisema ndugu huyo.


Mfugale ni miongoni mwa wamiliki wa hoteli wazawa aliyepata mafanikio katika biashara hiyo, akifungua hotel Dar es Salaam na nyingine mkoani Iringa.