Mmoja afa ajalini gari ikiteketea kwa moto

Tuesday June 28 2022
ajaliipiiic
By Hawa Mathias

Mbeya. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kunusurika katika ajali baada ya roli  lililobeba  shehena za mizigo likielekea mkoani Dar  es Salaam  kuferi breki na  kugonga magari  manne na kisha kuwaka moto katika  mtelemko wa barabara kuu ya Mbeya-Iringa eneo la Pipe line Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ,Urlich Matei amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu June 27, 2022 saa 12 asubuhi.

Amesema ajali hiyo ilihusisha roli la mizigo  likiwa linaendeshwa na Erick Ndasigwa (39) mkazi wa  Dar es Salaam  lilifeli breki na kisha kugonga magari manne likiwepo gari ndogo ambayo  dereva wake alipoteza maisha akiwa ndani ya gari.

Matei ametaja watu walionusurika katika ajali ani madereva akiwemo  aliyesababisha ajali , Erick Ntasigwa, Yunus Amos, Philimon Bartazali  na Abdafik Mohammed (29) mkazi wa jijini Mbeya na dereva wa Shirika Water Reed Tanzania

Matei amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mtelemko mkali uliopo kwenye eneo ilipotokea ajali

Matei ameomba Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kuangalia uwezekano wa kupanua miundombinu ya barabara kwa njia nne kutokana na kutumika katika usafirishaji wa shehena za mizigo kwenda nchi mbalimbali.

Advertisement

Wamesema  mara baada ya kufika eneo la tukio walikuta gari ndogo ikiwa imenasa chini ya roli la mizigo huku kukiwa na mwili wa mtu mmoja aliyeteketea kwa moto.

Advertisement