Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wateketeza bweni, wanafunzi walazwa kwa mshtuko

Sehemu ya chumba kilichounguzwa na moto katika shule ya Sekondari sabasaba iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kudhibiti moto uliokuwa ukitekekeza darasa lililokuwa likitumika kama bweli la wasichana katika shule ya sekondari ya Sabasaba ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mtwara. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema limefanikiwa kudhibiti moto uliokuwa ukitekekeza darasa lililokuwa likitumika kama bweli la wasichana katika shule ya sekondari ya Sabasaba ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 15 ofisini kwake mkoani hapa, Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa, Daniel Myalla amesema kuwa moto huo ulizua taharuki ambapo wanafunzi zaidi ya sita walikimbizwa hosptiali kutokana na mshtuko uliokakana na tukio hilo.

“Jana Agusti 14 majira ya saa 2.00 usiku tulipokea wito wa ajali ya moto katika shule ya sekondari Sabasaba iliyopo katika eneo la Chikongola Manispaa ya Mtwara Mikindani. 

“Tulifika eneo la tukio na kukuta wananchi na wanafunzi wa kiume wakipambana kuzima moto huo ambapo kwa hatua za awali walitumia maji kuukabili ule moto ambapo tulikuta sehemu kubwa ulikuwa tayari umedhibitiwa,” amesema.

Amesema walichofanya ni kuhakikisha kuwa majengo mengine matatu ya upande wa kushoto hayaathiriwi na moto huo ambayo ni majengo pacha na hilo linaloungua.

“Madhara yaliyojikeza ni pamoja na kuungua kwa madaftari, masanduku vitabu na vitu vya wanafunzi pamoja na  magodoro, kwani darasa hilo linatumiwa na wanafunzi wa kike kama bweni,” amesema.

Amesema kuwa wanafunzi wanne walipeelekwa hospitali ya Ligula na wengine wawili walipelekwa hospitali ya Likombe, lakini wote wameshatoka kwani ulikuwa ni mshituko tu.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, lakini bado uchunguzi unaendelea.

“Wakati unatokea wanafunzi walikuwa wapo darasani wakijisomea kabla hawajapata taarifa kutoka kwa mpita njia kuwa bweni la linateketea kwa moja,” amesema Myalla.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Zainab Juma, amesema kuwa watoto hao walipata mshtuko ambao ulipelekea kukimbizwa hosptiali kuhusu tukio hilo ambalo lilikuwa la ghafla na hawakuweza kuokoa vifaa vyao.

“Yaani hawa wanafunzi wamepoteza kil kitu wamebaki na nguo zao na madaftari machache ambayo ndio walikuwa nayo darasani wakisoma” amesema Zainab.