Moto wateketeza ghorofa Mwanza, lina maduka na makazi ya watu
Muktasari:
Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeibuka na kuteketeza jengo la ghorofa moja linalotumiwa na wafanyabiashara katika Mtaa wa Rwagasore katikati ya Jiji la Mwanza.
Mwanza. Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeibuka na kuteketeza jengo la ghorofa moja linalotumiwa na wafanyabiashara katika Mtaa wa Rwagasore katikati ya Jiji la Mwanza.
Pamoja na maduka, ghorofa hilo pia lina makazi ya watu na ghala linalotumiwa na wafanyabiashara wa vyombo vya muziki na vifaa vya simu kuhifadhi bidhaa zao.
Katika jengo hilo ambalo liko umbali usiyozidi Kilometa moja kutoka zilipo Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Mwanza kuna maduka ya wafanyabiashara wa vifaa vya simu (Electronics) na vyombo vya muziki.
Mashuhuda wanasema moto huo umeanza leo Jumatatu Oktoba 30, 2023 Saa 6:00 mchana huku wamiliki wakidai kuwa umeibuka kutokea eneo la juu la jengo hilo chanzo kikiwa hakijajulikana.
Bado Maofisa wa Zimamoto na Uokoaji wanaendelea na jitihada za kudhibiti moto huo usisambae katika majengo mengine.
Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi...