Moto wateketeza soko la mbao

Picha ya mtandao. Si ya tukio halisi
Muktasari:
Taarifa kutoka katika eneo la tukio zimebainisha kuwa gari la zimamoto la Mji wa Kahama limefika, lakini kutokana na moto kuwa mkubwa wameomba msaada kutoka kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Kahama. Soko la mbao lililoko Kata ya Majengo mjini Kahama limeteketea kwa moto pamoja na kuteketeza mali na vifaa mbalimbali.
Tukio hilo liloanza saa 12 jioni linadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme.
Taarifa kutoka katika eneo la tukio zimebainisha kuwa gari la zimamoto la Mji wa Kahama limefika, lakini kutokana na moto kuwa mkubwa wameomba msaada kutoka kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Soko hilo ambalo lipo karibu na stendi ndogo ya magari, limetengwa maalumu kwa ajili ya kuuzia mbao, kuranda na kuchomelea vifaambalimbal ivya chuma.
Hata hivyo, hakuna taarifa za majeruhi wala vifo katika tukio hilo. Jitihada za kuuzima moto huo zinaendelea.