Moto wateketeza soko Tunduma

Muktasari:
Soko la Manzese lililoko katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe linawaka moto muda huu.
Tunduma. Soko la Manzese lililoko katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe linawaka moto muda huu.
Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeanza leo Jumanne Novemba 16, 2021 asubuhi ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi wanaendelea kuuzima.
Soko hilo lina maduka ambayo yanauza bidhaa mbalimbali zikiwamo nguo, vipodozi, vifaa vya magari na viatu
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu wakati akiwa njiani kwenda kwenye soko hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songw, Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo akiahidi kutoa taarifa baada ya kufika kwenye soko hilo.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.