Mrema: Nimelipa Sh1 milioni mahari ya mke wangu

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema familia ya mke wake ilimtaka alipie mahari ya Sh4.2 milioni ambapo hadi sasa ameweza kulipa mahari ya  Sh1 milioni.


Moshi. Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema familia ya mke wake ilimtaka alipie mahari ya Sh4.2 milioni ambapo hadi sasa ameweza kulipa  Sh1 milioni.

Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urasi wa Tanzania, leo Alhamisi Machi 24, 2022 anafunga tena ndoa baada ya mke wake kufariki mwaka jana.

Mrema amesema aliwatuma wazee kwa familia ya mke wake mtarajiwa na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha mahari.

Maandalizi harusi ya Mrema yakamilika

Maandalizi kwa ajili ya harusi ya Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Mrema tayari yamekamilika tayari wamewasili katika kanisa katoliki parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro. Soma zaidi

VIDEO: Sababu za Mrema kutaka kuoa

Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Lyatonga Mrema ameelezea kilichomsukuma kuoa kuwa ni pamoja na kuepuka matamanio na kuzini kwa macho. Soma zaidi