Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshtuko, mfanyabiashara Bosco Chuwa afariki dunia

Mwonekano wa Nji wa Moshi, Kilimanjaro eneo alikofia mfanyabiashara, Bosco Chuwa.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Chuwa, kifo cha Chuwa kimetokea saa nne asubuhi, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC kwa ajili ya taratibu za kitabibu.

Moshi. Mfanyabiashara maarufu mjini Moshi anayemiliki kampuni ya ujenzi, Bosco Chuwa, amefariki dunia asubuhi ya leo Jumapili Julai 5,2026,  huku familia yake ikikanusha uvumi ulioenea kuwa alifia ndani ya gari nje ya baa moja maarufu eneo la Soweto.

Chuwa anamiliki kampuni ya Builders and Lime Works Construction Company Ltd inayotekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.

Habari za kifo chake zilianza kusambaa saa 10:00 jioni huku taarifa hizo zikidai kuwa alikumbwa na umauti akiwa ndani ya gari lake nje ya baa moja maarufu katika eneo la Soweto mjini Moshi, alipoliegesha baada ya kujisikia vibaya.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi leo Julai 5, 2026 kwa njia ya simu, ndugu wa marehemu, Hubert Chuwa, amethibitisha kifo hicho lakini akakanusha taarifa za kufia kwenye gari na kwamba alifariki akiwa nyumbani kwake.

Wakati ndugu yake huyo akisema taarifa za awali zinasema alifia nyumbani, taarifa nyingine zinadai alifia hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC wakati madaktari wakimhudumia wakijitahidi kuokoa maisha yake.

“Si kweli kwamba amefia ndani ya gari. Alikuwa nyumbani kwake hapa Moshi, ndipo alipofikwa na mauti,” amesema Chuwa.

Kwa mujibu wa Chuwa, kifo hicho kimetokea saa nne asubuhi, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC kwa ajili ya taratibu za kitabibu.

Chuwa, ameeleza kuwa marehemu alikuwa na changamoto za kiafya ambapo aliwahi  kupata kiharusi  ingawa aliendelea na maisha yake ya kawaida na shughuli za biashara kama kawaida.

Kuhusu mipango ya mazishi, amesema familia inaendelea na vikao vya ndani ili kuweka ratiba rasmi, huku mazishi yakitarajiwa kufanyika kijijini Uru, wilayani Moshi, ambako ndiko alikozikwa baba yake.

Amesema walikuwa na ushirikiano wa karibu kibiashara, wakitekeleza mradi wa ubia katika eneo la Ndungu wilayani Same ambao bado unaendelea.