Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MSLAC yawafikia waumini makanisani kutatua migogoro

Biharamulo. Waumini wa madhehebu ya kikristo katika halmashauri ya Wilaya Biharamulo wafikiwa na na timu ya wataalamu ya Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia makanisani  wakutuma wawakilishi kutatua migogoro mbali mbali kwenye jamii hadi makanisani.

Mkazi wa kijiji Msekwa kata Kalenge wilaya ya Biharamulo,Kasiri Mabula ambaye ni Muumini wa dhehebu la FPTC tawi la Msekwa akizungumza na mwananchi Digital,Leo 20 aprili,2025 amemtaja Rais Samia kama kiongozi aliyetukuka katika kutatua migogoro na kesi zinazojitokeza kwenye jamii.

"Aaah Rais mwenyewe kwanza tunamuombea kwa kadili alivyo kwasasaivi kasi yake tayari ya uongozi wake zamani tulikuwa tunafikilia kuwa huyu ni mwanamke tu lakini kwasasivi hata sisi wanaume anataka kutuzidi"

"Leo hii tayari miongozo ya huyu mama tayari amekuwa siyo mama tena ni mwanaume ambeye nu mama"amesema Kasiri

Kasiri, ameongoza kwa kusema  elimu ya msaada wa kisheria inayoendelea Nchini iliyowafikia kanisani na kijiini kwao itapunguza  kasi ya migogoro ya Urithi, Mirathi pamoja na Ndoa kujitokeza kwenye jamii.

Mkazi wa kijiji Msekwa, Kata Kalenge, Stella Mawazo amesema amefurahi kueleimishwa kukabiliana kisheria  na changamoto zilizokuwa zikijotokeza kijijini hapo.

Mchungaji wa kanisa la FPTC katika kijiji cha Msekwa,Mch.Jems Kayungilo amepongeza Timu ya msaada wa lisheria ya mama Samia kufika kanisani kwake na kutoa elimu ya msàda wa kisheria

Amesema wamepata elimu yeye na waumini wake wamefahamu namna ya kuepuka migogoro mbali mbali.

 Ameongeza kuwa, wanaendelea kumuombea kwa mwenyezi mungu yeye na timu yake aliyotuma nchi nzima kwa ajilb ya kusaidia wanajamii katika kupata suruhu ya migogoro.

Kwa upande wa mratibu mkuu Kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, Halmashauri ya wilaya Biharamulo mkoa Kagera, Salome Mwakalonge wakati akitoa semina kwenye makanisa mbali mbali amesisitiza waumini makanisani kutenda matendo mema na kuwa mabalozi wazuri kiimani wakutokomeza migogoro kwa kuikemea.

Amesema waumini wajenge tabia ya kufichua migogoro inayoweza kuhatarisha ustawi wa jamii kiuchumi maana sheria zipo wakiona jambo ambalo siyo sawa basi watoe taarifa sehemu husika kwa msaada zaidi.

Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imeanza kutekelezwa kwa kipindi cha siku kumu katika mkoa Kagera kwa halmashauti nane,upande wa wilaya Biharamulo imezifikia zaidi ya kata nane  tangu Aprili, 15 2025 na itakamilika mnamo Aprili, 24 2025 kwa kuzifika kata 10 na kila kata vijiji vitatu wananchi watapatiwq semina na kusikilizwa kero na changamoto zao  na Kampeni hiyo mpaka sasa imetolewa kitaifa katika mikoa 26.