Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtakuwa yapunguza ukatili wa kijinsia Rombo

Muktasari:

Wadau wa haki za binadamu, wananchi Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro wamesema kuanzishwa kwa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (Mtakuwa) umepunguza kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Rombo. Wadau wa haki za binadamu, wananchi Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro wamesema kuanzishwa kwa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (Mtakuwa) umepunguza kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wadau hao wa haki za binadamu wamesema matukio mengi ya ukatili yaliyokuwa yakifanywa Wilayani Rombo yanatokana na wananchi kutokuwa na elimu na kuamua kujichukulia sheria mkononi.

Mwenyekiti wa wasaidizi wa kisheria Wilaya ya Rombo, Remmy Shirima ,amesema  Kamati ya Mtakuwa iliyoanzishwa kwa ajili ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawke na watoto imesaidia sana kupunguza matukio ya ukatili kwenye jamii.

"Kamati hii imepunguza ukatili kwenye jamii kutokana na kuwa na wajumbe wengi kuanzia ngazi za kata hadi Mkoa kwahiyo jamii sasa  jamii  imeelimika na bado elimu inaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali ," amesema Shirima

Mkurugenzi wa shirika la kisheria na kutetea haki za binadamu (Ajiso)Mkoa wa Kilimanjaro ,Virginia Silayo amesema mpango huo wa  MTAKUWA umepunguza ukatili wa kijinsia kutokana  na elimu ya  ushirikishwaji kwa wadau wa ngazi mbalimbali za jamii.

"Nashauri Mtakuwa awamu ya pili itakayoanza mwakani na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa mafunzo kwenye kamati za Mtakuwa ianzie ngazi za vijiji kwasababu awamu ya kwanza tumefanya zaidi kwenye mikoa na Halmashauri na kidogo kwenye Kata,"alisema Silayo

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Lesorroma,Adolfina Atanasi amesema mwanzoni kabla hawajapata elimu hiyo walikuwa wanaogopa kutoa ushirikiano pale tukio la ukatili linapojitokeza kwenye jamii kutokana na hofu.

"Sasa hivi baada ya kupata hii elimu ya Mtakuwa tumekuwa wajasiri kwasababu tumeelewa mambo mengi juu ya ukatili wa kijinsia na hii inatupa fursa ya kutoa ushirikiano pale ambapo panapotokea ukatili tunaripoti kwa haraka kwa wahusika,"alisema Adolfina

Mpango huo ambao ulianzishwa mwaka 2018 ulilenga kupunguza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.