Mtoto apata saratani ya damu, aomba msaada wa tiba

Muktasari:
Baba mzazi wa mtoto huyo, Elibariki Nnko amesema kuwa mtoto wake huyo amegundulika kuwa na saratani ya damu, hivyo anatakiwa kumpelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Mtoto Josephat Nnko mwenye umri wa miaka 10 na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kwatulele ambaye ni mkazi wa King’ori mkoani Arusha, anaomba msaada wa kwenda kutibiwa saratani ya damu nchini India.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Elibariki Nnko amesema kuwa mtoto wake huyo amegundulika kuwa na saratani ya damu, hivyo anatakiwa kumpelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Akizungumza leo Februari 27 mjini Moshi, Nnko amesema kwamba mtoto wake huyo alianza kuugua mwaka 2016 na alizidiwa Oktoba 2017, ambapo alianza kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Amesema katika jitihada za madaktari wa KCMC kumpatia mtoto huyo matibabu wamebaini kuwa ana saratani ya damu na ndipo alipotakiwa kumsafirisha nje ili aweze kutibiwa.
Amesema gharama za kusafiri pamoja na matibabu ni Sh50 milioni ambapo amesema kutokana na shughuli anayofanya ya kujipatia kipato na familia inayomtegemea hana uwezo wa kupata kiasi hicho cha fedha.
Hivyo, anawaomba Watanzania wamsaidie kumchangia gharama hizo ili mwanaye aweze kuendelea na masomo hadi kufikia ndoto zake. Kwa yeyote atakayeguswa
anaweza kumchangia kupitia namba 0744-455042 ELIBARIKI NNKO