Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto wa miaka miwili achinjwa, mtuhumiwa auawa

Eneo ambapo yamefanyika mauaji ya mtoto wa miaka miwili, Ivani Colomani ambaye ameuawa kwa kuchinjwa katika Kijiji cha Ngumbaro Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

Mtoto Ivani Colomani (2) amefariki dunia baada ya kuchinjwa katika Kijiji cha Ngumbaro Kata ya Songu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro huku anayedaiwa kufanya mauaji hayo naye akiuawa.

Siha.

Mtoto Ivani Colomani (2) amefariki dunia baada ya kuchinjwa katika Kijiji cha Ngumbaro Kata ya Songu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro huku anayedaiwa kufanya mauaji hayo naye akiuawa.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Aprili 18, 2022 mchana katika Kijiji hicho ambapo anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo, Jumanne Athumani (63) naye amefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa matukio hiyo na kuekeza kuwa tayari ametuma kikosi cha polisi kwenye eneo la tukio.

"Taarifa za tukio hilo nimezisikia na nimetuma polisi kufuatilia ili kupata taarifa sahihi za tukio hilo" amesema Kamanda Maigwa.

Ndugu wa mtoto hyuo, Julius Gasper amesema mtoto huyo alikuwa na wenzake watatu wakicheza lakini baada ya muda hakuonekana.

Gasper amesema alianza kumtafuta mtoto huyo ambapo alikuta kiatu chake nyumbani kwa jirani yao huku mlango ukiwa umefungwa na damu zikichuruzika kutoka ndani.

"Baada ya kuona vile nilisogea karibu na kuanza kusukuma kwa nguvu mlango ulipofunguka niliona damu zimetapakaa hapo ndani na kupiga kelele za kuomba msaada, tulikuta huyo mzee akiwa na panga mkononi alikuwa anemchinja mtoto na kumuweka kwenye kiroba".

Diwani wa Kata hiyo, Joachimu Makundi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngumbaro amesema kuwa mzee anayedaiwa kufanya tukio hilo ni mganga wa kienyeji.

"Ni kweli nilikuwa Lawate nimepigiwa simu kwamba kuna mauaji yametokea, nimefika nimekuta ni kweli, nikawapigia simu polisi kituo cha Sanya Juu, wamefika na kuuchukua mwili wa marehemu kuupeleka chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali ya Kibongoto ".

"Lakini pia huyo aliyemchinja mtoto, naye amefariki kutokana na kipigo cha wananchi, na mwili wake pia tumeuhifadhi hapo Hospitali ya Kibongoto"amesema Makundi