Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtumbwi wazama, waua watatu Ziwa Victoria

Muktasari:

  • Mtumbwi huo ulikuwa na madumu 33 ya maji.

Muleba. Watu watatu wamekufa maji  ndani ya Ziwa Victoria katika Kisiwa cha  Ilamba wilayani Muleba baada ya mtumbwi kuzama.

Watu hao walikuwa wakitoka kuchota maji Kisiwa cha Mazinga. Mwili mmoja umeshaopolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema watu hao walizama jana Jumatatu saa 6:30 mchana.

Amesema miili ambayo haijapatikana ni ya Superius Severine (27) mkazi wa Kijiji cha  Nyakitaba na Evelius Zephrine (22) wa Mubunda Kitoko wilayani Muleba

Kamanda Olomi amesema mwili uliopatikana ni wa Adela Andrea (26),  mkazi wa Kijiji cha Itongo.

Amesema Nelson Boniphace (20), mkazi wa Kisiwa cha Ilamba aliogelea na kuokolewa.

Mtumbwi huo uliokuwa na madumu 33 ya maji amesema unamilikiwa na Rashidi Sabini (33), mkazi wa Kijiji cha Ilamba.

Amesema mtumbwi huo kutokana na upepo ulipigwa na wimbi hivyo ulipinduka na kuzama.