Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtwara watahadharishwa na mafuriko

Muktasari:

  •  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas ameagiza wananchi wanaoishi katika maeneo yanayojaa maji kuchukua tahadhari ya mvua za El- Nino

Mtwara. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas ameagiza wananchi wanaoishi maeneo yanayojaa maji kuchukua tahadhari ya mvua za El- Nino zinazotarajia kunyesha mkoani hapa kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 23, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisema yapo maeneo maarufu kwa kujaa maji, likiwamo la Kiyangu.

“Tunatarajia kufanya maboresho ya miundombinu, lakini ni muhimu kuwatahadharisha hasa wanaoishi katika maeneo korofi ambayo mvua ikinyesha yanajaa maji," amesema Kanali Abbas.

Pia, Kanali Abbas amesisitiza kufanyika maandalizi ya kilimo kwa wakulima kupanda mazao mchanganyiko kwa ajili ya biashara na chakula Ili kuweza kuzitumia vizuri mvua hizo.

“Tumeshafungua msimu wa kilimo maofisa kilimo wanapaswa kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kulima mazao mbalimbali yatakayowasaidia  kwa chakula na biashara Ili kukuza uchumi wa familia na mkoa Kwa ujumla," amesema Kanal Abbas.

Meneja wa TMA Mkoa wa Mtwara, Elewa Msomba amesema wananchi wanapaswa kufuatilia taarifa za hali ya hewa kila siku.

Mkazi wa Kiyangu, Mwajuma Shabani amesema eneo hilo linajaa maji kwa sababu mtaro uliochimbwa kuelekea baharini haujakamilishwa kwa muda mrefu.