Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yachelewesha makarani wa sensa Dar

Muktasari:

  • Mvua iliyoanza kunyesha asubuhi ya leo Jumapili, imekuwa miongoni mwa sababu zilizowafanya makarani wa sensa kuchelewa kufika baadhi ya maneneo jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mvua iliyoanza kunyesha asubuhi ya leo Jumanne, Agosti 23, 2022 imechangia kuchelewa kwa makarani wa sensa katika baadhi ya mitaa jimbo la Mbagala.

 Kama ambavyo ilitangazwa, sensa itaanza asubuhi ya Agosti 23, 2022  wakazi wa kata ya Toangoma waliokuwa wamejiandaa kuhesabiwa wamejikuta wakisubiri kwa muda kabla ya kuanza kutembelewa na makarani.

Akizungumza na Mwananchi, Ester Mangachi amesema aliamka mapema akisubiri karani apite ila hadi saa 2:40 asubuhi bado hajahesabiwa.

“Nilikuwa nataka wanikute mwenyewe ila naona mvua imeleta changamoto kidogo, sasa mie wacha nikatafute riziki kwanza, watawakuta wengine maana taarifa zote nimeacha,” amesema Ester.

Akizungumzia hali hiyo, msimamizi wa makarani, mtaa wa Mzinga B, Onesmo Bundi amesema changamoto ya kuchelewa iliyojitokeza imetokana na mvua.

“Tumeona leo kumekucha na mvua ndio maana kuna sehemu makarani wamechelewa kufika ila kazi inaendelea na tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wakuu wa kaya.

“Nimeshazungumza na makarani wangu kubeba miamvuli maana hatujui hali itakuwaje kwa kutwa nzima, hatutaki sisi kuwa kikwazo lazima kazi ifanyike,” amesema Bundi.