Mwalimu Kashasha afariki dunia

Mwalimu Kashasha afariki dunia

Muktasari:

  • Mchambuzi wa soka maarufu nchini, Alex Kashasha maarufu Mwalimu Kashasha amefariki dunia leo Agosti 19, 2021 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Mchambuzi wa soka maarufu nchini, Alex Kashasha maarufu Mwalimu Kashasha amefariki dunia leo Agosti 19, 2021 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo Kashasha alikuwa akifanya kazi limethibitisha taarifa hiyo na juhudi za kutafuta familia yake zinaendelea.

Mwalimu Kashsha alikuwa miongoni mwa wachambuzi wa gazeti la Mwanaspoti Jumamosi.

Kwa habari kamili endelea kufuatilia Mwananchi.