Mwanafunzi auawa kwa deni la Sh3000

Muktasari:

  • Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Suye jijini Arusha, Evance Florian (17) ameuawa kwa kipigo ikielezwa kuwa chanzo ni deni la Sh3000.


Arusha. Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Suye jijini Arusha, Evance Florian (17) ameuawa kwa kipigo ikielezwa kuwa chanzo ni deni la Sh3000.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Novemba 14, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo amesema mwanafunzi huyo amefariki jana akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru na akifafanua chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo ni kupigwa.

Amesema jeshi hilo linamshikilia mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha, Ibrahim Shaban (18) kwa madai ya kumpiga kijana huyo Florian na kumsababishia kifo.

Kamanda Masejo amesema uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika jarada litafikishwa katika ofisi ya mashitaka kwa hatua za kisheria.

Amesema mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mount Meru .