Mwanafunzi bora kidato cha nne anatoka familia ya wasomi

Mwanafunzi bora kidato cha nne anatoka familia ya wasomi

Muktasari:

  • Paul Luziga ni mtoto wa tano katika familia ya Luziga na ndugu zake wawili wamehitimu chuo kikuu na wengine wawili  wanasoma katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Dar es Salaam. Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2020, Paul Luziga aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Panda Hill ya jijini Mbeya anatoka familia ya wasomi.
Paul ni mtoto wa tano katika familia ya Luziga na ndugu zake wawili wamehitimu chuo kikuu na wengine wawili  wanasoma katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Angalia matokeo hapa
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Januari 15, 2021 mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Lucy Mwogela amesema siri ya watoto wake kufanya vizuri shuleni ni kumwamini Mungu.
Watoto hao wote wamefika chuo kikuu wakisomea fani mbalimbali.

Matokeo ya kidato cha nne 2020/2021 haya hapa


“Mtoto wa kwanza alimaliza shahada ya kwanza yuko Dar es Salaam anafanya kazi. Wa pili ni wa kike amemaliza shahada ya uzamili, watatu na wa nne ni mapacha wapo chuo kikuu na huyu Paul ndiyo wa mwisho.”
“Siri ni kumwamini Mungu tu, hakuna ujanja wowote ninaoweza kufanya,” amesema Lucy.