Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanafunzi Chuo cha Polisi afariki ajali ya pikipiki

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa

Muktasari:

  • Mwanafunzi wa mafunzo ya awali wa Shule ya Polisi Tanzania (TPS), Stanford Stanley (22) amefariki dunia na wengine 7 kujeruhiwa, baada ya kugongwa na pikipiki wakati wakiwa kwenye mazoezi ya mchakamchaka.

  

Moshi. Mwanafunzi wa mafunzo ya awali wa Shule ya Polisi Tanzania (TPS), Stanford Stanley (22) amefariki dunia na wengine 7 kujeruhiwa, baada ya kugongwa na pikipiki wakati wakiwa kwenye mazoezi ya mchakamchaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea leo Jumanne Februari 1, 2022 saa 10 alfajiri, katika eneo la barabara ya Lema kata ya Kilimanjaro Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kamanda Maigwa ameeleza kuwa, pikipiki hiyo aina ya Boxer ikiendeshwa na Vitalis Mushi (43) mkazi wa Longuo Manispaa ya Moshi, akitokea Moshi mjini kuelekea Shanty Town iliwagonga watembea kwa miguu hao ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Polisi Moshi olisi Tanzania, wakati wakiwa kwenye mazoezi ya mchakamchaka asubuhi na kusababisha kifo na majeruhi.

Amewataja majeruhi hao ambao wameumia sehemu mbalimbali za miili yao kuwa ni Baraka Boniface (22), Bakari Modestus (22), George Masanja (20), Hassan Hija (21), Halima Abdi (22), Robina Samson (22) na Vitalis Mushi (43) ambaye ndiye mwendesha pikipiki hiyo, ambayo iliwagonga na kusababisha kifo na majeruhi.

Aidha kamanda amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mwendesha pikipiki, ulevi na kushindwa kuchukua tahadhari kwa watembea kwa miguu.

"Mwendesha pikipiki huyo ambaye ameumia kichwani, mkononi na mguu, amekutwa na kiwango kikubwa cha ulevi 405mg/100ml, baada ya kupimwa na upelelezi zaidi unaendelea na utakapokamilika atafikishwa mahakamani," amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda amewataka watumiaji wa vyombo vya moto, kuacha kutumia vileo wakati wanapotumia vyombo hivyo.