Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenyekiti Uvccm Kagera aja na kauli 'Mtaa hautaki Digree wala PhD kuonekana mchapa kazi'

Karagwe. Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa Kagera, Faris Buruhan amesema mtaa hautaki digree wala PhD ili uonekane kijana mchapa kazi.

Kauli hiyo ameitoa leo Machi 12, 2025 katika Chuo cha Serikali, Veta Karagwe wakati akizungumza na wanachuo wa chuo hicho kuhusu umuhimu wa elimu ya ufundi stadi wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa Kagera.

"Mtaa hautaki digree, mtaa hauitaji PhD, mtaa hauitaji Falsafa na vitabu vingi bali mtaa unataka watu wa kuendesha mitambo kwenye viwanda"

 "Nchi imewekeza kwenye viwanda na wanaofanya kazi kwenye mitambo siyo watu wenye masters ni watu wenye elimu maarifa na ufundi" amesema

Amewataka vijana kusoma kwa bidii elimu ya ufindi nchini na  kufanya kazi kulingana na fani walizosomea bila kujali ukubwa wa elimu ya watu waliyowazunguka.

Faris, amesema kwa sasa Elimu ya ufundi ndiyo kimbilio kwa vijana hakuna haja kwa wale waliyopo vyuo vya kati na ufundi stadi kujitizama kinyonge niwakati wa vijana wanaosoma kozi za ufundi katika vyuo vya veta kujiona kama mashujaa wanaolipigania  taifa.

Chuo hicho kina wanafunzi 336 na nikati ya vyuo vya Veta hapa  nchini ambavyo Serikali imewekeza fedha kuendeleza na kukarabati miundombinu ambapo Sh4.6 bilioni zimetumika kukarabati madarasa na kununulia vifaa vya kujifunzia.