Mwenyekiti wa CCM mkoani Simiyu afariki dunia

Tuesday February 23 2021
Mwenyekiti pic
By Mwandishi Wetu

Bariadi. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo amefariki dunia leo asubuhi Jumanne Februari 23, 2021 nyumbani kwake Mwanuzi wilayani  Meatu.

Taarifa ya kifo chake zimetolewa na katibu mwenezi wa chama hicho mkoani humo, Mayunga George, “CCM mkoa wa Simiyu tunasikitika kutangaza kifo cha mwenyekiti wetu wa mkoa, Enock Yakobo  kilichotokea leo. Taratibu za mazishi zitatolewa baadaye baada ya kukaa na familia.”

Advertisement