Mwigulu: Msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Mwigulu: Msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Muktasari:

  • Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani kuacha tabia hiyo kwa maelezo kuwa fedha zao haziwezi kuchukuliwa.

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani kuacha tabia hiyo kwa maelezo kuwa fedha zao haziwezi kuchukuliwa.

Dk Mwigulu ameeleza hayo leo Jumamosi Aprili 3, 2021 katika kikao na watendaji wa wizara hiyo na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Msajili wa Hazina (TR).

Mwigulu: Msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

 “Kwa wale wafanyabiashara walioona wakiweka fedha zao zitaonekana mtandaoni labda zitachukuliwa zote nitoe rai warudishe fedha kwenye mabenki zitaliwa mchwa au panya bila sababu,  uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi.”

“Kodi itatozwa tu kwa sehemu ya fedha inayotakiwa kukusanywa na sisi tujenge utaratibu wa kutii sheria kulipa kodi na kuwa wazalendo kwa nchi yetu.” Amesema Mwigulu.