Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa Mtanzania aliyeuawa Israel wakwama

Muktasari:

  • Mwili huo ambao uliagwa nchini Israel Novemba 22, 2023 na kushuhudiwa na baadhi ya Watanzania, awali ulitarajiwa  kuwasili leo Jumamosi na baadaye maziko kufanyika siku ya Jumanne ya Novemba 28; 2023; nyumbani kwao katika Kijiji cha Kirwa Mashati, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro. Sasa unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu.

Moshi. Mwili wa Clemence Mtenga (22) Mtanzania aliyeuawa nchini Israel, haukuwasili nchini leo kama ilivyokuwa imeelezwa hapo awali, na badala yake unatarajiwa kuwasili Jumatatu, Novemba 27, 2023 saa 2 usiku, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

 Mwili huo ambao uliagwa nchini Israel Novemba 22, 2023 na kushuhudiwa na baadhi ya Watanzania, unatarajiwa kuzikwa Jumanne ya Novemba 28 nyumbani kwao katika kijiji cha Kirwa Mashati, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Jana Novemba 24, 2023; Boniphace Mtenga ambaye ni msemaji wa familia hiyo alisema kuwa mwili wa Clemence ungewasili nchini leo Jumamosi Novemba 25, na kutahifadhiwa katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo, kusubiri taratibu za maziko.

Akizungumza kwa simu leo Novemba 25, 2023 Mtenga ambaye pia ni mwenyekiti wa ukoo huo, amesema mwili huo umeshindikana kuwasili leo, baada ya ndege iliyokuwa iulete kusitisha safari zake, na hivyo kwa sasa wanatarajia kuupokea siku ya Jumatatu.

“Ndege ambayo ilikuwa ilete mwili wa Clemence nchini, imesitisha safari zake hivyo kwa sasa tumepewa taarifa kuwa mwili utaingia nchini saa zilezile lakini siku ya Jumatatu, Novemba 27, mwaka huu,” amesema.

Ameongeza kuwa “Tumeambiwa kwa sasa mwili uko Uholanzi, hivyo tunaendelea kuusubiri, na endapo utafika Jumatatu kama tulivyoelezwa, ratiba ya maziko itakuwa palepale siku ya Jumanne, Novemba 28, mwaka huu."

Novemba 17, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Clemence Mtenga, ambaye ni miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo baada ya kuanza kwa vita kati ya Hamas na Israel.

Taarifa hiyo iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano ya Serikali cha wizara hiyo, ilieleza Clemence alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania 260, waliokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo, chini ya mpango wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi hiyo.