Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa mtoto waopolewa ajali ya mitumbwi Bunda

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiuandaa mwili wa mtoto uliopolewa kutoka ndani ya maji ya Ziwa Victoriai. Picha na Beldina Nyakeke 

Muktasari:

  • Ajali ya kuzama kwa mitumbwi miwili iliyobeba abiria 28 ilitokea Julai 30, 2023 baada ya kupigwa na dharuba kali.

Bunda. Mwili wa mtoto wa kike ambaye ni kati ya watu 13 waliozama majini baada ya mitumbwi miwili kuzama ndani ya Ziwa Victoria katika pwani ya Kijiji cha Mchigondo Wilaya ya Bunda umeopolewa.

Mwili huo umeopolewa Saa 7:25 mchana wa leo Jumanne Agosti Mosi, 2023 na vikosi vya uokoaji vinavyoundwa na Askari wa Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi Kikosi cha Maji na wavuvi, siku tatu tangu ajali hiyo itokee.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema kasi ya uokozi imeongezeka leo baada ya kuwasili kwa boti mbili za kisasa (fiber) na askari wazamiaji 22 kutoka mikoa ya Mara na Mwanza.

‘’Licha ya changamoto kadhaa ikiwemo hali mbaya ya hewa, kina kirefu na mkondo wa maji unaoenda kasi, vikosi vyetu vya uokoaji vinafanya kila linalowezekana kuopoa miili ya wote wanaohofiwa kuzama majini,’’ amesema Magere

Mkuu wa Mkoa Mara, Said Mtanda ameahidi kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi ya wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyoacha simanzi kwa wakazi wa vijiji vya Kata ya Igundu.

"Serikali italipigia gharama za kusafirisha miili ya wapendwa wetu kwenda sehemu ambayo familia itaamua kufanya mazishi pamoja na ubani wa Sh1 milioni kwa kila familia," amesema

Mkuu huyo wa mkoa amesema japo matumaini ya kuwapata waliozama wakiwa hai inazidi kufifia kutokana na muda uliopta tangu ajali itokee, nia ya Serikali ni kufanya kila linalowezekana miili yote ipatikane na kuzikwa kwa heshima.

Ajali ya kuzama kwa mitumbwi miwili iliyobeba abiria 28 ilitokea Julai 30, 2023 baada ya kupigwa na dharuba kali.

Abiria wote, watu wazima na watoto ni waumini wa Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK) waliokuwa wakitoka kwenye ibada Kijiji cha Mchigondo.

Mitumbwi yote miwili ilikuwa inaenda Kitongoji cha Bulomba kilichoko Kijiji cha Igundu Wilaya ya Bunda mkoani Mara