Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali mbaya ya hewa yakwamisha uokoaji waliozama Ziwa Victoria

Baadhi ya ndugu wa watu 13 wanaohofiwa kufariki dunia baada ya mitumbwi yao miwili kuzama dani ya Ziwa Victoria wakishuhudia ndugu zao wanavyotafutwa majini.

Muktasari:

  • Kazi ya ukozi wa watu 13 wanaohofiwa kufariki dunia baada ya mitumbwi waliyokuwa wakusafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Bunda. Kazi ya ukozi wa watu 13 wanaohofiwa kufariki dunia baada ya mitumbwi waliyokuwa wakusafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Watu hao walikumbwa na tukio hilo walipokuwa wakitoka Kijiji cha Mchigondo kwenda Kijiji cha Igundu walikoenda kuhudhuria ibada katika Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK), ndipo ajali hiyo ikatokea Saa 12:30 jioni ya  Julai 30, 2023.

Kazi hiyo imesitishwa  kutokana sababu mbalimbali ikiwemo hali mbaya ya hewa, kukosekana kwa  vifaa na zana za kisasa za uokozi.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema leo Julai 31, 2023 katika kijiji cha Mchigondo ambapo kazi hiyo inafanyika kuwa  tayari wamefanya jitihada kadhaa kuhakikisha kuwa watu hao wanatolewa ziwani.

"Tumewasiliana na wenzetu wa jeshi la polisi wana maji Mwanza ambao tayari wametoa boti ya kisasa (fiber) na tayari iko njiani inakuja kuongeza nguvu hapa,"amesema

Amesema kuwa  upepo mkali katika eneo hilo, giza na tope jingi ndani ya maji ni miongoni mwa changamoto ambazo wazamiaji wamekumbana nazo hivyo kufanya kazi hiyo kuwa ngumu.

"Upepo sasa hivi ni mkali na mkondo wa maji unaenda kasi, unakwenda kwa kasi sana ," amesema

Baadhi ya ndugu wa watu waliozama majini wameiomba Serikali kuongeza  nguvu ili ndugu zao waweze kupatikana na hatiamaye hatua  zingine ziweze kufanyika.

"Hivi kweli kwa kutumia boti hizi za ndoano unategemea hii kazi itakamilila kweli, tunaomba Serikali ilete vifaa vya kisasa ili jambo hili liweze kukamilika," amesema Nyanjura Magafu

Akizungumzia majeruhi wa ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bunda amesema watu 14 waliookolewa na kukimbizwa kwa matibabu katika Hospitali ya Kibara hali zao zinaendelea vizuri na tisa kati yao walitarajiwa kuruhusiwa kurejea nyumbani.

"Hapa tunavyoongea majeruhi  tisa wataruhusiwa kutoka hospitalini kwasababu hali zao zinaendelalea vizuri," amesema Dk Naano

Manusura wa ajali hiyo, Baraka Jumbula amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha waumini  kanisa hilo ambao walifika katika kijiji cha Mchigondo kwaajili ya ibada maalum ya kupanga mipango mikakati ya mahubiri yanayotarajiwa kuendeshwa na kanisa hilo katika eneo la Iramba wilayani Bunda.

Amesema kuwa wakiwa wamefika katikati ya safari mtumbwi mmoja ulipigwa na dhoruba ndipo walipoomba msaada kwenye mtumbwi mwingine na walipofika kwaajili ya kuwaokoa ndipo mitumbwi yote ikazama kabla ya kupata msaada kutoka mtumbwi mwingine.

Mwenyekiti wa kijiji cha Igundu, Sumila Nyamkinda amesema kuwa mitumbwi hiyo ilikuwa imebeba watu 28 ambapo hadi sasa mwili wa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja ndio umeopolewa.

"Tumepoteza watu 13 ambao walikuwa miongoni mwa waumini waliokuja hapa kijijini kusali na hadi sasa jitihada za kuwatafuta zinafanyika, “amesema