Mwili wa Tarimo kuwasili Januari 26

Mwanafunzi wa kitanzania, Raymond Tarimo akiwa nchini Urusi enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Dada wa marehemu, Salome Kisale amesema taarifa za uhakika kuhusu kuwasi kwa mwili wanatarajia kuzipata kesho Januari 26, 2023.

Dar es Salaam. Wakati mwili wa Mtanzania aliyefia nchini Russia, Nemes Tarimo ukitoka nchini humo, familia yake imesema utawasili nchini kuanzia kesho Januari 26 na utasafirishwa kwenfa Tukuyu mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi.
Nemes aliyekuwa akisoma nchini Russia aliuawa Oktoba 24, 2022 wakati akiwa vitani Ukraine akipigana kuisaidia Russia kupitia kundi la Wagner.
Akizungumza na Mwananchi leo Januari 25, dada wa marehemu, Salome Kisale amesema taarifa za uhakika kuhusu kuwasi kwa mwili wanatarajia kuzipata kesho Januari 26, 2023.
"Jana mwili uliondoka Moscow na sasa uko Uturuki kwa hiyo tunatarajia kesho ndo tutapewa taarifa kamili kuhusu siku na muda wa kuwasili.
"Baada ya mwili kuwasili Tanzania tutakuja hapa nyumbani kwao Mbezi na taratibu zote ikiwemo kusoma wasifu wa marehemu, kuaga na chakula zitafanyika hapa, kisha tutakua na safari ya kwenda kumpumzisha katika kijiji cha Kasyetokata ya Msasani wilayani Tukuyu mkoani Mbeya," amesema.