Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzumbe yaingia ushirikiano na mamlaka ya ega kuboresha mitaala kimtandao

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa William Mwigoha na  
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Salum Rugambwa wakisaini mkataba wa makubaliano wa mambo manne ambayo yatatekelzwa na Chuo Kikuu Mzumbe lengo likiwa ni kufanya maboresho ya mitaala na ufanisi kwa chuoni hapo. Lilian Lucas

Muktasari:

  • Mzumbe itafanya maboresho kwenye eneo la ujifunzajaji na maeneo kadhaa namna ambavyo wanafunzi na walimu watapata kueleza zaidi na wataenda kufanyakazi eGA na kuona namna wanaweza kutumia uzoefu kwa ajili ya kuboresha mitaala ya chuo.

Morogoro. Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro  kimesaini mkataba wa ushirikiano na mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania eGA wenye lengo la kufanya kazi kwa pamoja  ili kuleta mabadiliko katika mfumo wa ufundishaji wa kimtandao.

Chuo Kikuu Mzumbe ni Taasisi ya Elimu ya 15 inayojiunga na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA) ambayo itasaidia kuleta chachu na mabadiliko ya kiutafiti katika vyuo vikuu kwa njia ya mtandao

Ushirikiano huo umefanyika Oktoba 18, 2023 chuoni hapo Mzumbe mbele ya menejimenti ya Chuo na baadhi ya viongozi kutoka eGA.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa William Mwigoha amesema kama chuo waliangalia maeneo muhimu ya kuingia ushirikiano huo nia ikiwa ni katika kuboresha mitaala na kuongeza ufanisi.

"Baada ya kupata maeneo muhimu ya kushirikiana na eGA sasa tumeweza kusaini makubaliano na sasa watatengeneza mpango kazi wa kuendelea kutekeleza, mambo muhimu tuliokubaliana ni pamoja na eneo la ufundishaji ambalo litafanyiwa mabadiliko ya namna ya kutoa ufundishaji kwa kwenda kimtandao zaidi.

Amesema tayari wametengeneza mifumo ndani ya chuo ambayo itahakikisha itasaidia kutoa elimu kwa njia ya mtandao kwani eGA wana mifumo hiyo tayari lakini wamekuwa wakiangalia namna inavyotakiwa kuendesha mifumo hiyo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya eGA, Salum Rugambwa amesema Chuo Kikuu Mzumbe kimeona umuhimu wa kushirikiana na mamlaka hiyo baada ya kupata mafunzo ya masuala ya mtandao serikalini na kuona manufaa yaliyopo.

Amesema hatua ya kuingia makubaliano kwenye maeneo mbalimbali lengo ni kuhakikisha jitihada zinaendelezwa na kuzaa matunda moja wapo ya uthamani wa eGA ni kuwa na ushirikiano.
Rugambwa amesema eGA imekuwa kila mwaka inachukua wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali na kuja kufanya mafunzo kwa vitendo na bunifu na mpaka sasa mamlaka imeshaingia mikataba kama hiyo kwa vyuo vikuu 14 na Chuo Kikuu Mzumbe ni cha 15.