Ndege ya Precision Air yapata ajali ziwani Bukoba

Picha ya ndege ya Shirika la Precision Air imepata ajali katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha taarifa za ajali hiyo.

Dar es Salaam. Ndege ya Shirika la Precision Air imepata ajali katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera. 

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumapili 6, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha taarifa za ajali hiyo na kusema kuwa yupo kwenye eneo la tukio akiendelea na uokoiaji.

“Iko sahihi hiyo taarifa niko kwenye eneo la tukio nafanya uokozi, siwezi kuzingumza zaidi” amejibu kwa kifupi Kamnda Mwampaghale alipopigiwa simu.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha ndege hiyo ikiwa imetumbukia kwenye maji.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa ndege hiyo imepata ajali jirani na Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Hata hivyo bado hakuna taarifa za ndege hiyo ilikuwa ina abiria wangapi na ilikuwa inekwenda wapi


Endelea kufuatilia Mwananchi