Ndugai amwapisha Dk Stergomena

Ndugai amwapisha Dk Stergomena

Muktasari:

  •  Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemuapisha mbunge wa kuteuliwa, Dk Stergomena Lawrence Tax leo Ijumaa Septemba 2021.


Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemuapisha mbunge wa kuteuliwa, Dk Stergomena Lawrence Tax leo Ijumaa Septemba 2021.

Ndugai amemuapisha Tax baada ya kuteuliwa leo na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Dk Stergomena anakuwa mbunge wa tisa kuteuliwa na rais na idadi hiyo inafanya nafasi ya uteuzi alizopewa kikatiba kubaki moja.

Kabla ya uteuzi huo, Stergomena alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti 2021.

Ndugai amemuapisha kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Ndugai amesema amefanya hivyo mara baada ya kupokea taarifa ya uteuzi kutoka kwa Rais Samia.

Amempongeza kwa kazi kubwa ya kuwa Katibu Mtendaji SADC,”nasikia fahari kubwa kuwa miongoni  mwetu karibu nyumbani,”amesema.