Rais Samia afanya uteuzi

Friday September 10 2021
uteuzipic

Dk Stergomena Tax

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 10, 2021 amemteua Dk Stergomena Tax kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema Tax ameteuliwa kutoka kwenye nafasi kumi za wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye amemaliza muda wake mwezi Agosti 2021.

Mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma zaidi: Rais Samia afanya uteuzi

Advertisement