Rais Samia afanya uteuzi

Tuesday August 17 2021
uteuzi pc
By Anna Potinus

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othamn aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha cha Ardhi (ARU).

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Agosti 17, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu imesema pia Rais Samia pia amemteua Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Profesa Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Soma hapa: Samia ateua mabalozi 23, yupo Hoyce Temu

Profesa Ole Gabriel anachukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu.

Profesa Ole Gabriel ataapishwa Agosti 21 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam pamoja na mabalozi wateule watatu ambao ni: 
Balozi mteule Luteni Jenerali Yakub Hassan Mohamed aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.

Balozi mteule Mahmoud Thabit Kombo aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Balozi Mteule Elsie Sia Kanza aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Advertisement
Advertisement