Samia ateua mabalozi 23, yupo Hoyce Temu

Muktasari:

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amefanya uteuzi wa mabalozi 23 akiwemo mlimbwende wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amefanya uteuzi wa mabalozi 23 akiwemo mlimbwende wa Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu.

Hoyce Temu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Mei 22, 2021 na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza imewataja mabalozi hao wapya kuwa ni Luteni Jenerali Yakub Mohamed, Meja Jenerali Richard Makanzo, Pereira Ame Silima, Maulidah Hassan na Togolani Mavura.

Wengine ni Edwin Rutegaruka, Fredrick Kibuta, Noel Kaganda, Mindi Kasiga, Caroline Chipeta, Macocha Tembele, Agnes Kayola, Masoud Balozi, Ceasar Waitara, Swahiba Mndeme pamoja na Said Mshana.

Pia Rais Samia amewateua Alex Kallua, Mahmoud Kombo, James Bwana, Said Mussa, Elsie Kanza pamoja na Robert Kahendaguza.

“Uteuzi wa Mabalozi hawa umeanza leo Mei 22, 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye,” imesema taarifa hiyo.