Ndugulile aanza ziara ya siku tatu Arusha

Ndugulile aanza ziara ya siku tatu Arusha

Muktasari:

  • Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile ameanza ziara ya siku tatu mkoa wa Arusha kukagua utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Arusha. Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile ameanza ziara ya siku tatu mkoa wa Arusha kukagua utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Akiwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha leo Jumanne Machi 16, 2021 alikutana na kaimu katibu tawala wa Mkoa, Agnery Chitukulo.

Amesema akiwa mkoani Arusha atatembelea ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Kaskazini na ofisi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Kesho waziri huyo atakagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la shirika la umoja wa Posta barani Afrika na atakabidhi hati ya uwanja katika eneo utakapofanyika ujenzi.

"Tanzania ni mdau muhimu katika kuhakikisha makao makuu ya umoja wa Posta yanakua hapa nchini, awali kulikuwa na sintofahamu,” amesema.