NEC: Serikali imeendesha uchaguzi mkuu kwa fedha zake asilimia 100

Saturday August 21 2021
kupigakurapic
By Zourha Malisa

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage amesema kwa mara ya kwanza Serikali ya Tanzania imeboresha  daftari la kudumu la wapiga kura na kuendesha uchaguzi mkuu kwa asilimia 100 bila ya kutegemea msaada.

Amezungumza hayo leo Jumamosi Agosti 21, 2021 katika hafla ya kukabidhi taarifa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam.

Amesema Serikali iliendesha uchaguzi bila kutegemea msaada na kwa mujibu wa sheria,   fedha zilizotumika zililipwa kutoka mfuko mkuu wa Hazina.

Amesema NEC  katika kipindi cha uchaguzi ilifanya maandalizi ya bajeti kwa awamu mbili ambapo  Sh154.3 bilioni ya awamu ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

“Fedha hizo pamoja na mambo mengine zilitumika kugharamia ununuzi wa vifaa vya uboreshaji, uchapishaji wa nyaraka mbalimbali, mafunzo kwa watendaji wa uboreshaji na utoaji wa elimu ya mpigakura, " amesema.

Ameeleza kuwa bajeti ya awamu ya pili ilikuwa ni uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo Sh262.5 bilioni zilitumika kuendesha shughuli hiyo.

Advertisement

“Zilitumika kugharamia shughuli mbalimbali za uchaguzi ikiwemo ununuzi wa vifaa na huduma kama  karatasi za kura, masanduku ya kura uchapishaji wa nyaraka mbalimbali, mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi  na elimu ya mpiga kura."

“Kwa mujibu wa kifungu 122 cha sheria ya Taifa ya uchaguzi kikisomwa pamoja na kifungu cha 120 cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa fedha zilizotumika kuboreshaji, " amesema.

Advertisement