Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Necta yampa matumaini mwanafunzi aliyenasa saa 24 ndani ya kifusi Kariakoo

Jackson Clement mwanafunzi wa kidato cha Nne. Picha Azam TV

Muktasari:

  • Wanafunzi wa kidato cha nne wanaendelea na mitihani ya mwisho hadi Novemba 29, 2024 itakapohitimishwa, akiwemo Clement aliyenusurika kwenye ajali ya ghorofa lililoporomoka Kariakoo, anayeiomba Necta imsaidie kufanya mtihani alioukosa.

Dar es Salaam. Ombi la Jackson Clement, mwanafunzi wa kidato cha nne aliyenusurika kifo kwenye ajali ya ghorofa Kariakoo, limesikika baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) kumhakikishia hatapoteza haki yake.

Clement ni miongoni mwa manusura wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne, Kariakoo jijini Dar es Salaam, lililosababisha vifo vya watu 16 na majeruhi zaidi ya 86 na uharibifu mali za mamilioni ya shilingi Novemba 16, 2024.

Jana Jumanne, Novemba 19, 2024, Clement ambaye ni mwanafunzi wa sekondari ya Charambe, alisimulia kisa chake kuwa huwa anakwenda kumsaidia shemeji yake siku za mwisho wa wiki, na kuwa siku anakutwa na mkasa huo alikwishafanya mitihani saba ya kuhitimu kidato cha nne.

“Biology mmoja bado practical, nilikuwa na ombi kwa mwalimu wangu atafute namna yoyote ili nisaidiwe niweze kuufanya mtihani,” alisema Clement akiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOl) anakoendelea na matibabu.

Mitihani ya kidato cha nne, ilianza Novemba 11 na itamazika Novemba 29, 2024.

Leo Jumatano, Novemba 20, 2024, Mwananchi limemtafuta Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Ally Mohamed kufahamu hatima ya maombi ya Clement, na kuwajibiwa kuwa mwanafunzi huyo hatapoteza haki yake ya kumaliza mtihani wake wa mwisho.

Dk Mohamed amesema baraza litatumia kanuni zake katika kushughulikia suala hilo na mwanafunzi huyo hatapoteza haki yake ya mtihani. 

Amesema jana Jumanne alimtembelea mwanafunzi huyo kumjulia hali na kumhakikishia atapata haki hiyo ya kufanya mtihani huo uliobaki.

“Ni mwanafunzi ambaye alikuwa na juhudi, ajali imetokea na yeye ikamkuta, lakini baraza litampa haki yake kadri inavyostahiki,” amesema.

“Baraza lina taratibu zake litaandaa taarifa zake na kuchukua hatua stahiki. Lakini niseme tu, tumefarijika kuona katika mitihani yake ya wiki ya kwanza ameweza kufanya yote na alikuwa anatarajia kufanya mtihani wa Practical Biology 2B tarehe 21 amesema Mohamed.

Endelea kufuatilia Mwananchi