Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NHC yaongeza mapato yake kufikia Sh257 bilioni

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

Muktasari:

  • Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeongeza mapato yake kutoka Sh144.42 hadi kufikia Sh257 .47.

Dar es Salaam. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeongeza mapato yake kutoka Sh144.42 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021  hadi kufikia Sh257 .47 mwaka 2022.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Februari 1,2023  na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nehemia Mchechu, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kuelezea ufanisi wa shirika hilo na mwelekeo wake kwa mwaka 2022/2023.

Mchechu alisema mapato hayo yameongezeka kutoka vyanzo mbalimbali vya shirika ikiwemo kodi kutoka kwa wapangaji wao, uuzwaji wa nyumba zao, kushiriki katika kazi za ukandarasi ambapo wao ni makandarasi daraja la kwanza na kazi za ushauri.

"Msingi wa mapato wa NHC siku zote ni kujikita katika kufanya biashara na sio kutegemea ruzuku na ndio imesababisha matunda yote haya katika kuongezea mapato," amesema Mchechu.

Pia amesema sababu zingine ni kuimarika kwa sera za nyumba na sekta ya nyumba nchini ambapo ni kipaumbele cha Rais Samia Suluhu Hassan kuona sera hizo zinaenda zaidi kwenye sekta binafsi.

Akifafanua zaidi kuhusu mapato hayo amesema kwa mapato yatokanayo na kodi  yamepanda kutoka Sh89.23 hadi kufika Sh90.76 bilioni.

Kadhalika  mapato ya mauzo ya nyumba yamepanda kutoka Sh29.33 mwaka 2021 na kufikia Sh121.95 bilioni kwa mwaka 2022.

Huku mapato miradi ya ukandarasi yamekuwa kutoka Sh25.60 bilioni na kufika Sh43.98 bilioni kwa mwaka huo 2022.

Hata hivyo Mchechu  alisema kwa upande wa faida halisi inayotokana na  Shirika iliongezeka hadi kufikia Sh60.7 bilioni kutoka sh 31.7 bilioni mwaka 2021.

"Ongezeko hili linaendana na sambamba na ongezeko la majengo na hali ya nyumba pia imeanza kuimarika  hivyo ni matarajio kwa mwaka 2022/2023 shirika  litaendelea kupata faida kubwa,"alisema Mkurugenzi huyo.

Akielezea mwelekeo wa shirika mwaka 2023 Mchechu amesema ni kuendelea kukamilisha miradi iliyokuwa imesimama ukiwemo wa Morocco Square  ambao ujenzi wake upo kwenye hatua za mwisho kukamilika

"Mikakati mingine ni kuendelea kukusanya madeni, kutekeleza miradi ya ubia kwa kushirikiana na sekta binafsi na kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya  kuzifanyia nyumba zao matengezo zipato 18,622 kote nchini.