Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NIMR yashauri kuunganisha matibabu ya kisukari na VVU

Muktasari:

  • Taasisi ya Taifa ua Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeshauri huduma za matibabu ya kisukari ziunganishwe na kliniki za watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WaVVU).

Dodoma. Taasisi ya Taifa ua Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeshauri huduma za matibabu ya kisukari ziunganishwe na kliniki za watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WaVVU).

Ushauri huo umetolewa kutokana na utafiti uliofanyika kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2022 katika wilaya za Magu, Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza kuonyesha kuwa tatizo la ugonjwa wa kisukari ni kubwa kwa WaVVU kuliko wasiokuwa na maambukizi ya VVU.

Akizungumza leo Alhamis Juni 2,2022 Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya amesema kuungwanishwa kwa kliniki hiyo kutasaidia kupunguza usumbufu na gharama.

Aidha, ameshauri mazoezi ya mwili yawe ni sehemu ya tiba katika kliniki za wanaoishi na VVU.

“Isichukuliwe kuwa mazoezi ya mwili ni hiari ya mtu iwe ni sehemu za tiba, upewe dawa za kufubaza lakini ikiwezekana ufanyishwe mazoezi kama wewe huwezi kuamua kufanya mazoezi iwe ni sehemu ya tiba,”amesema

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Seif Shekilaghe amesema wizara yake imekuwa ikitoa fedha  kwa ajili ya kuhakikisha mchango wa tafiti unafanyika kupitia katika taasisi.

“Chini ya NIMR tafiti mbalimbali za magonjwa ya binadamu zinafanyika ili tuweze kupata majibu mazuri na kuondoa matatizo haya katika jamii yetu,”amesema.

Naye Mtafiti wa Mkuu katika utafiti huo kutoka NIMR, Dk George Praygod amesema katika nchi za Afrika kulionekana hakuna takwimu zinazowashawishi wanaotunga na kubadilisha sera ili kuhakikisha huduma za magonjwa yasiyoambukiza zinaweza kuunganishwa na HIV.

“Ili kuweza kuziba pengo hilo ndio maana tuliamua kufanya utafiti huu ili kuweza kutoa ushahidi kuwa tatizo lipo na vyombo vinavyohusika vinatakiwa kuchukua hatua ili huduma za matibabu yasiyoambukiza na huduma HIV waweze kuhudumiwa vizuri na matokeo yake kuwa mazuri,”amesema.