NIT ni kitovu cha mafunzo ya sekta ya usafirishaji Tanzania na nchi jirani

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu ambapo ili kulitimiza ni lazima kuwekeza kwenye sekta muhimu kama viwanda.

Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu ambapo ili kulitimiza ni lazima kuwekeza kwenye sekta muhimu kama viwanda.

Hii ni kutokana na kwamba, kuanzisha viwanda, kunakuza uchumi, kutengeneza ajira kwa wananchi na hivyo kuwawezesha kuwa na kipato cha kukidhi mahi-taji yao na familia zao.

Pia, kutokana na kipato watakachopata, Serikali itakuwa na wigo mpana wa kukusanya kodi. Vilevile wananchi wataweza kumiliki mali zisizohamishika, kama ardhi, majengo na hivyo kuiwezesha Serikali kupata kodi katika mali hizo.

Hapa ndipo lengo la kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya watu linapoonekana kutimia. Hata hivyo yanahitajika kujengwa mazingira mazuri ili kuhakikisha dhamira hiyo inafanikiwa. Mojawapo ya mazingira hayo ni kuwa na sekta imara ya usafiri.

Sekta imara ya usafiri itatengeneza mazingira rahisi katika muktadha wa usafirishaji wa malighafi kutoka shambani kwenda viwandani na kutoka viwandani kwenda sokoni.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hivyo, kutokana na umuhimu huo ni lazima kuweka mikakati ya kuhakikisha sekta hiyo inakuwa imara ili kukidhi mahitaji haya ya mapinduzi ya kiuchumi.

Katika kuhakikisha suala la usafiri nchini linafanikiwa, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) chini ya ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali kimejipanga kuhakikisha kinaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri kwa kufundisha wataalam wa kada mbalimbali za sekta hiyo.

Naibu Mkuu wa Chuo cha NIT-Mipango, Fedha na Utawala, Dk Zainabu Mshana anasema taasisi hiyo ambayo ni mahali sahihi pa kupata mafunzo ya kozi mbalimbali hususani usafiri ilianza mwaka 1975 kama idara inayotoa mafunzo kwa madereva na watu wanaofanya shughuli za usafirishaji chini ya Shirika la Usafirishaji la Taifa.

Anasema mwaka 1982 ilion-ekana kwamba idara ya usafirish-aji inakuwa hivyo kuna uhitaji mkubwa wa mafunzo ili kupata wataalamu zaidi hivyo kupitia sheria ya bunge ya mwaka 1982 Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilianzishwa na kupewa ithibati ya kutoa mafunzo ya usafirishaji katika nyanja zote tano ambazo ni; barabara, anga, reli, maji na chini ya ardhi (pipeline).

“Kama zilivyo taasisi za elimu ya juu NIT ina majukumu ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa mujibu wa sheria ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2009,” amesema Dk Zainabu.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Anasema mwaka 1982 wakati chuo kinaanza, kilikuwa na pro-gramu mbili pekee zilizokuwa zikiishia ngazi ya Stashahada (Diploma) na wanafunzi 500 wakaongezeka mpaka 700 lakini mpaka sasa chuo kina programu zaidi ya 30 ambazo zimeanzia ngazi ya Astashahada (certificate) mpaka Shahada ya Uzamivu (Masters) na wanafunzi zaidi ya 12,000.

Anasema pia kuna kozi za muda mfupi kwa ajili ya maendeleo ya kitaaluma, katika masuala ya anga, kozi za udereva na wahudumu wa ndege (cabin crew).

Dk Zainabu anasema kutokana na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia katika sekta ya usafirishaji kuna hitaji kubwa la wataalamu wengi watakaosaidia Taifa kuendana na mabadiliko hayo hivyo NIT imejipanga kuhakikisha inakwenda sambamba na mabadiliko hayo.

“Kwa mzazi au mlezi anayehitaji kumleta mtoto wake kusoma NIT matarajio yetu ni kwamba atakachokipata kimuwezeshe kufikia malengo yake kwa sababu hata mikakati ya nchi kimaendeleo imelipa kipaumbele eneo la usafirishaji kwa sababu ndiyo mhimili wa uchumi na maendeleo,” anasema Dk Zainabu.

Anasema kwa sasa Taifa lina uhitaji mkubwa wa wataal-amu wa usafiri wa njia ya anga, reli, maji na ardhi kutokana na uwekezaji uliofanyika kwenye maeneo hayo hivyo NIT wapo kwa ajili ya kuisaidia Serikali kupata wataalamu hao kwa kutoa mafunzo bora yanayoendana na mabadiliko ya kiuchumi na teknolojia.

“Kwa sasa tuna programu ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege (Aircraft Maintenance Engineering) ambayo ina mwaka wa tatu inatoa wahitimu ambao wengi wapo kwenye viwanja mbalimbali vya ndege na wengine wanafanya mafunzo ya vitendo ndani na nje ya nchi mfano mwaka huu mwanafunzi mmoja amepata nafasi ya kufanya mafunzo hayo kwenye kampuni ya Kenya Airways,hii inadhihirisha namna NIT ilivyokuwa sehemu sahihi,” anasema Dk Zainabu.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Anasema NIT ina wakufunzi waliobobea ambao wanahakiki-sha mhitimu baada ya kumaliza masomo yake anakuwa ameka-milika kuingia kwenye soko la ajira kutokana na mafunzo bora ambayo wanayatoa.

Anasema katika mwaka wa masomo 2022/2023 NIT inawakaribisha waombaji wote kuchagua chuo hicho kwani ndiyo kitovu cha mafunzo ya sekta ya usafiri Tanzania na nchi jirani.

“Kwa sasa dirisha la kwanza la udahili limefungwa na kuna amboa wamefanya maombi kwenye dirisha hilo, nataka kuwaambia kwamba tunawashukuru na kuwakaribisha NIT kwani wamechagua sehemu sahihi. Kwa ambao bado hawajafanya maombi dirisha la pili limesha-funguliwa na udahili unaendelea wafanye maombi tunawakaribi-sha sana,” anasema Dk Zainabu.

Akieleza kuhusu kozi zinazoitofautisha NIT na taasisi nyingine Dk Zainabu anasema kuna kozi kama vile; Aircraft Maintenance Engineering, Logistics and Transport Management, Railway Logistics Management. Kozi zote hizi zinatolewa na NIT pekee hapa nchini.

Kuhusu idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa na chuo hicho Dk Zainabu anasema kwa sasa chuo kinapokea wanafunzi wengi kulinganisha na miaka ya nyuma hii ni kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika katika masuala kama uwepo wa vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia, miundombinu bora na wataalamu wabobevu wa kutosha.

Kwa upande wa tafiti Dk Zainabu anasema mpaka sasa chuo hicho kimefanya tafiti zaidi ya asilimia 70 za usafirishaji ambazo zimetumika kwenye maeneo mbalimbali nchini na zimeweza kutatua changamoto nyingi katika jamii.

Kuhusu changamoto Dk Zainabu anasema kubwa ni upungufu wa mabweni ambapo kwa sasa wanaishughulikia kwani kwa kujenga mabweni yatakayotosha idadi ya wanafunzi na katika kulitekeleza wamepata ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mradi wa The East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) ambao kwa sasa umeanza na mabweni mawili ambayo yata-chukua wanafunzi 750 kila moja.

Vijana wanatakiwa kuchan-gamkia fursa ya kwenda NIT kwa sababu sekta ya usafiri inakuwa kwa kasi na ina uhitaji mkubwa wa rasilimali watu hivyo kusoma kozi hizo watajitengenezea mazingira mazuri ya kupata ajira na kujiajiri wenyewe.