Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Njaa yamtoa mafichoni mtuhumiwa wa mauaji, akamatwa

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera William Mwampaghale akizungumza na waandishi wa habari leo, Februari 21,2023 juu ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa mauaji

Muktasari:

  • Mtuhumiwa wa mauaji ya Hadija Ismail aliyekaa mafichoni kwa siku sita amekamatwana jeshi la polisi baada ya kuumwa njaa iliyompelekea kujitokeza hadharani kuomba chakula.

Bukoba. Paschal Kaigwa Mariseli (21) mkazi wa mtaa wa National housing kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba anayetuhumiwa kwa mauaji ya Hadija Ismail (29) amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Kagera baada ya kukaa mafichoni kwa siku sita.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na jeshi la polisi Jumapili Februari 19, 2023 baada ya kutoka mafichoni alikokuwa amejificha baada ya kuumwa njaa iliyomtoa kwenda kuomba msaada wa chakula nyumbani kwa shanghazi yake mtaa wa Kashai Katotorwansi manispaa ya Bukoba.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, Wiliam Mwampaghale amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa wanaendelea kumuhoji mtuhumiwa ili jeshi hilo liweze kukamilisha upepelezi kwa ajili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

“Mtuhumiwa wa mauji ya Hadija Ismail tumemkamata Februari 19,2023 majira ya saa 10:00 jioni baada ya kutekeleza mauji Februari 13,2023 na kwenda kujificha katika vichaka kwa muda wote huo na baada ya njaa kali aliamua kutoka mafichoni kwenda kwa shanghazi yake Kashai Katotorwansi kuomba chakula alipofika nyumbani shanghazi yake hakuwepo amewakuta watoto waliokuwa wanamfahamu ambao baada ya kumuona wamepiga kelele na majirani wamefika na kumkamata,” Amesema Mwampaghale.

Ikumbukwe kuwa, kijana huyo anayetuhumiwa kwa mauaji alikuwa anaishi na marehemu nyumba moja baada ya mume wa marehemu ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa National housing Manispaa ya Bukoba, David Dominick kumchukua na kuishi naye kama mwanafamilia akifanya shughuli za ujenzi akishirikiana na mwenyekiti tangu Novemba,2022.

Tukio la mauji lilitokea Februari 13,2023 majira ya saa 12:00 jioni ambapo mtuhumiwa alimpiga marehemu kwa kutumia silaha butu kichwani upande wa kushoto na kumsababishia jeraha kubwa lililopelekea kuvuja damu iliyomsababisha umauti papo hapo na kisha kumbaka na baada ya kutekeleza tukio hilo aliondoka na kuelekea kusikojulikana hadi alipojitokeza hadharani juzi Jumapili.