Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyangumi asafiri kilomita 13,000 kutoka Colombia kufuata wenza Tanzania

Tovuti ya Shirika la Habari la Uingereza (BBC) limeripoti kuwa nyangumi mmoja amesafiri kwa umbali wa kilometa 13,000 kutoka Colombia na kufika Tanzania kwa ajili ya kutafuta wenza na kujilinda na mabadiliko ya tabianchi.

“Wanasayansi wanasema alionekana Bahari ya Pasifiki karibu na nchi ya Colombia mwaka 2017, kisha kuzuka tena miaka kadhaa baadaye kisiwani Zanzibar katika Bahari Hindi.

“Wataalamu wanaamini kuwa safari hii ya umbali wa kilomita 13,000 inaweza kuwa imesababishwa na mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha kupungua kwa hifadhi za chakula au safari ya kutafuta wenza,” imeripoti BBC.

 Mtaalamu kutoka kwenye programu ya mamalia wa baharini nchini Tanzania, Ekaterina Kalashnikova amesema tukio hilo ni la kushangaza na la kipekee hata kwa aina hii ya wanyama wanaohama sana.

Nyangumi huyo mwanaume pia aliwahi kuonekana katika pwani ya Pasifiki nchini Colombia mwaka 2013.

Alitambuliwa tena katika eneo hilo mwaka 2017 na kuonekana kando ya Bahari ya Hindi visiwani Zanzibar mwaka 2022.