Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofisa TRA afariki kwa kujirusha ghorofani

Muktasari:

  • Richard Walalaze ni miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya Mamlaka hiyo ya mwaka.

Tanga. Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Arusha, Richard Walalaze (35) amekutwa amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani jijini Tanga.

 Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mfanyakazi huyo amejirusha kutoka ghorofa ya pili ya Hoteli ya Ocean Breez jijini Tanga alikokuwa amepanga chumba tangu Julai 16 mwaka huu.

Mwananchi imefahamishwa kuwa Richard alikuwa miongoni mwa watumishi wa TRA waliokuwa jijini Tanga kwa kazi maalumu ya kuandaa taarifa ya Mamlaka hiyo ya mwaka.


Kwa habari zaidi endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yetu kwa habari zaidi.