Oryx Gas Tanzania Limited na miaka mitatu ya uwekezaji kukuza maendeleo ya soko la Gesi ya kupikia (LPG)

Oryx Gas Tanzania Limited na miaka mitatu ya uwekezaji kukuza maendeleo ya soko la Gesi ya kupikia (LPG)

Muktasari:

  • Kiongozi wa soko la usam-bazaji wa gesi kwa ajili ya matumizi ya majumba-ni (LPG) nchini Tanzania, Oryx Gas Tanzania Limited (“OGTL”, Kampuni ya Oryx Energies) inapanga kufanya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania kusaidia juhudi za serikali katika kukuza matumizi ya LPG ikiwa ni gesi safi na rafiki kwa mazingira ya kupikia na kwa shughuli za kibiashara / viwanda.

Kiongozi wa soko la usam-bazaji wa gesi kwa ajili ya matumizi ya majumba-ni (LPG) nchini Tanzania, Oryx Gas Tanzania Limited (“OGTL”, Kampuni ya Oryx Energies) inapanga kufanya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania kusaidia juhudi za serikali katika kukuza matumizi ya LPG ikiwa ni gesi safi na rafiki kwa mazingira ya kupikia na kwa shughuli za kibiashara / viwanda.

Uwekezaji huu wa baadaye utajikita katika usambazaji wa mitungi ya gesi, uboreshaji wa miundombinu mipya na mitambo na bohari za gesi zilizopo.

Akizungumza na vyombo vya habari katika mahojiano maalum wiki hii, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Benoit Araman alisema kuwa Oryx Gas Tanzania Limited (OGTL) inaangalia sekta ya nishati ya Tanzania kama mkakati wa kwanza muhimu ambapo kuna mahitaji mengi ya kufanywa kuhakikisha Watanzania wanapata nisha-ti salama, ya kuaminika, fanisi na nafuu kama vile LPG ambayo inafaa matumizi ya nyumbani, biashara na viwanda.

“Kampuni ya Oryx Gas Tanzania ina hakika kuwa LPG, ambayo kiwango chake cha kupenya katika soko la gesi nchini ni asilimia 5 pekee, inaweza kufanikiwa kukuza soko hilo ambalo kwa ujumla wake ukuaji wake ni asilimia 5 tu.

Ndiyo maana kwa uzoefu wetu wa kutoa huduma wa muda mrefu na ushiriki katika kujenga uaminifu na sekta za Umma na Binafsi katika sekta ya nishati, tumeendelea kuwekeza katika miundombinu, mitungi ya gesi na uhamasishaji wa wateja kutumia na kuona faida ya bidhaa zetu,” alisema.

Benoit alisema OGTL kwa sasa inaendesha bohari 8 za LPG na mitambo ya kujaza gesi nchini ambayo inaruhusu kampuni hiyo pamoja na njia zake za usambazaji wa LPG, kufikia sehemu kubwa ya nchi ikiwamo pamoja na maeneo ya vijijini.

Aliongeza zaidi kuwa anaipongeza serikali kwa juhudi inazofanya katika kuutoa uchumi sehemu moja na kuufanya unufaishe zaidi tabaka la wa watu wa kati. Aliongeza kuwa uwekezaji wa sasa na Serikali katika miundombinu una faida kubwa kwa nchi na mfano mzuri ni bandari ya Dar es salaam ambayo imewekwa kama moja ya bandari kuu ya Afrika Mashariki, ambayo uwekezaji umefanywa na sasa inahitaji vifaa vya kisa-sa vya ziada, fanisi ikiwa ni pamoja na nguvu kazi yenye ujuzi ili kupunguza msongamano wa sasa wakati ina-saidia ukuaji wa nchi.

Kwa uwepo wake nchi-ni kwa zaidi ya miaka 20 na kiwango cha uwekezaji wa zamani, wa sasa na wa baadaye, Oryx Energies inathibitisha kujitoa kwake kwa muda mrefu hapa Tan-zania na imani yake kubwa katika maendeleo yake. Ikiwa imetengeneza moja ya majukwaa makubwa zaidi na yaliyounganishwa ya sekta ya nishati, na ikiongoza mnyororo wa thamani kutoka kwenye ununuzi wa bidhaa halisi kwenye soko lililo wazi kupitia kampuni yake ndogo ya biashara (Addax Energy) hadi katika uhifadhi, uchanganyaji wa bidhaa, usambazaji na usimamizi wa shughuli nzima katika eneo la uzalishaji ambao ndiyo unaohitajika zaidi, Oryx Energies inakusudia kukidhi mahitaji ya nishati ya wateja na biashara kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa kutoa bidhaa na huduma za kuaminika na bora, pamoja na mafuta, ikiwamo LPG na vilainishi vikichagizwa na mfumo wake fanisi wa usafirishaji, mitandao ya usambazaji thabiti, pamoja na vituo vya huduma kwa wateja.

Oryx Energies ikiwa ni mshirika mwenye weledi na wa kuaminika wa biashara amejikita katika mfumo ulio-jumuishwa wa uchakataji nishati ya gesi hadi inapom-fikia mlaji wa mwisho ambao unaiwezesha kampuni kud-hibiti mnyororo wa thamani kwa kutafuta bidhaa kutoka kwenye soko la wazi kupitia kampuni yake ndogo ya biashara hadi uhifadhi na usambazaji wao wa kimkaka-ti hadi kuwafikia watumiaji wa mwisho.

Ikijivunia njia zake bora za usafirishaji na mitandao thabiti ya usambazaji, pamoja na vituo vyake vya hudu-ma kwa wateja na huduma maalum ya ujazaji magari ya kusafirisha gesi na mafuta kukidhi mahitaji ya wateja walio ukanda wa pwani, Oryx Energies hutoa bidhaa na huduma mbalimbali kama vile mafuta, gesi ya kupikia majumbani (LPG) na vilainishi inavyovizalisha yenyewe. Tangu mwaka 1989, kampuni hiyo imeanzisha vituo kadhaa vikubwa vya utunzaji mafuta na gesi kote Afrika Mashariki na Magharibi, pamoja na Dar es Salaam (Tanzania), Calabar (Nige-ria), Freetown (Sierra Leone), Cotonou (Benin) na Dakar (Senegal).

Vituo hivi vinaun-ga mkono lengo la kampuni la usambazaji wa kuaminika wa bidhaa na huduma za mafu-ta kwa mataifa yaliyo ukanda wa pwani na zaidi, nchi ambazo hazina bahari.

Oryx Energies ni mojawapo ya watoa huduma wakubwa, wakongwe na wanaojitegemea wa bidhaa na huduma za mafuta na gesi kwa Afrika, kampuni hii inazalisha, inauza, inahifadhi na inasambaza bidhaa za mafuta na gesi zinazohitajika na wateja, biashara na shughuli za baharini katika nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kundi la kampuni za Uswisi, nyingi zikiwa zinamilikiwa na kundi la makampuni ya uwekezaji la AOG, Oryx Energies leo iko katika nchi zaidi ya 20 za Kusini mwa Jangwa la Sahara, na imekuwa ikiendana na mahitaji ya nishati yanayokua ya ukanda huo kwa zaidi ya miaka 30. Oryx Energies imekuwa mstari wa mbele kusaidia na kuwawezesha wanawake katika kuhakikisha wanafikia malengo yao na kuwa sehemu ya wachangiaji wa ukuaji wa uchumi.

Uwekezaji mkubwa wa kampuni hiyo huchochea mchango mkubwa wa maendeleo ya kijamii katika miradi mbalimbali kwa ukanda wote hususan katika nyanja zote za kijamii kusaidia serikali na watu kupata huduma bora za kijamii.