Pingamizi jingine kesi ya kina Mbowe

Tuesday November 30 2021
mbowepic
By Hadija Jumanne
By James Magai

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka umewasilisha mapingamizi matatu kupinga kupokewa kwa vielelezo vya shahidi wa pili katika kesi ndogo ndani ya kesi ya kubwa ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Akitoa mapingamizi hayo leo Jumanne Novemba 30, 2021 wakili wa Serikali mwandamizi, Robert Kidando ameeleza kuwa pingamizi la kwanza ni kuhusu nyaraka mbalimbali  na barua kwa hakimu mkazi Kisutu kutohusika  na shauri hilo dogo lililopo mahakamani hapo.

Mawakili wa Serikali wakiwasilisha mapingamizi yao:

Baada ya mawakili wa Serikali kukagua nyaraka hizo na kujadiliana kwa muda mfupi, Wakili Kidando anasimama na kusema:Mheshimiwa Jaji tunapingamizi kuhusiana na upokelewaji wa nyaraka hizo alizozileta shahidi wa pili.

Wakili Kidando: Pingamizi letu la kwanza nyaraka proceedings, charge sheet na barua kwa Hakimu Mkazi Kisutu hazina relevance na shauri hili dogo.

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji kuhusiana na nyaraka hizi pia tuna cha kuelezea kuhusiana na hiyo hati ya mashtaka. Kilicholegwa mahakamani hapa ni copy ambayo kwa mujibu wa sheria copy haiwezi kupokewa kabla ya kukidhi vigezo vya sheria kama vilivotajwa kuanzia kifungu cha 65, 66 na 67 cha Sheria ya Ushahidi.

Advertisement

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji kuhusiana na dispatch sahidi aliyeko mahakamani lazima awe competent kuweza kuitoa hapa mahakamani.

Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji sisi tuko tayari kuendelea kutoa submissions na ataanza Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla.

Jaji Tiganga: Kwa hiyo mapingamizi ni matatu, siyo?

Kidando: Ndio Mheshimiwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Hilla anaanza kutoa hoja:

Wakili Hilla: Kuhusiana na relevance (kuwa na uhusiano) Mheshimiwa Jaji nyaraka ambayo wenzetu wanataka kui-tender ukizitizama nyaraka zote hizo zonahusiana na criminal case namba 77/20 Kati ya Jamhuri na Lembrus Mchome iliyokuwa katika Mahakama ya Kisutu.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji hakuna namna yoyote ile nyaraka hizi zinahusiana na shauri hili lililoko mbele yako. Hakuna mamna yoyote ile Mheshimiwa Jaji nyaraka hizi zinahusiana na DC Msemwa  ambaye ni PW2 (shahidi wa pili upande wa mashtaka) katika shauri hili dogo.

Wakili Hilla: Nyarama Mheshimiwa Jaji hazina uhusiana na hoja ya DC Msemwa kuwepo Central Police na hata Oysterbay Police. Nyaraka Mheshimiwa hazina indicator yoyote ile kwamba DC Msemwa aliwahi kufanya kazi mwezi Mei 2020 katika kituo cha Polisi Oysterbay.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji nyaraka hizi pia hazina uhusiano na ukamatwaji wa Ling'wenya na uandikwaji maelezo ya Ling'wenya wala kuonesha kwamba Lembrus Mchome DW2 (shahidi wa pili wa utetezi) amewahi kukaa kituo cha Polisi Oysterbay.

Wakili Hilla:  Mheshimiwa Jaji kwa mujibu wa section 7 ya Sheria ya Ushahidi, ni kwamba ushahidi Mheshimiwa Jaji utatolewa na kupokewa mahakamani kama uko relevant na si vinginevyo.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji mahakama yako hii ni mahakama ya sheria  kwamba kila kinachofanyike kwa mujibu wa sheria na lazima kiwe na connection, kiwe na uhusiano na jambo lililopo.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji hii kesi ya DPP vs Sharif Mohamed Athuman na wenzake 6 Criminal Appeal number 84/2016 ukurasa wa sita aya ya mwisho na page Seven, Mahakama ya Rufani inasema kwamba fact inakuwa relevant Kama inakusudia ku-prove ama disapprove jambo husika.

Wakili Hilla: Mheshimiwa bila kuwepo mipaka hiyo mahakama inaweza kuletewa mambo mengi yasiyo na msingi

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji, barua inayotaka kuletwa mahakamani, inatoka Tan Africa Law imesainiwa na wakili Peter Kibatala imeelekezwa kwa Hakimu Mkazi Kisutu kwanza imenakiliwa kwa Lembrus Mchome na Depute Registrar wa Mahakama hii, wanaomba proceedings za kesi hiyo namba 77 iliyokuwa Kisutu.

Wakili Hilla: Barua haimtaji Ling'wenya, wala haiongelei ukamatwaji wa Ling'wenya

Wakili Hilla: Ni kwamba barua haiongelei jambo lolote lililo hapa mahakamani.

Wakili Hilla: Kibaya zaidi Mheshimiwa Jaji DW2 hajaieleza mahakama namna gani anahusiana na Ling'wenya, hajaongelea namna gani hii barua inahusiana na ukamatwaji Ling'wenya.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji DW2 hajaeleza namna gani barua hii, proceedings na dispatch namna gani vinahusiana na yeye kuwepo pale Oysterbay Police.

Wakili Hilla:  Mheshimiwa Jaji charge hii inahusiana na pornography, inaeleza kuwa shahidi huyu alikamatwa kwa kupiga picha kiongozi wa taasisi fulani, akashtakiwa kwa matumizi maovu ya mtandao.

Wakili Hilla: Swali la kujiuliza, shauri hili linahusiana namna gani na haya mashtaka ya matumizi mabaya ya mtandao. Yana uhusiano gani na kupiga picha kiongozi wa taasisi fulani

Wakili Hilla: Yana uhusiano gani na DC Msemwa?  yana uhusiano gani na DC Msemwa kuwepo Oysterbay Police. Nyaraka zinatakiwa ziongee zenyewe. Ni submissions yetu kuwa nyaraka hizi haziongei the fact issue iliyoko hapa mahakamani.

Wakili Hilla: Ushahidi wake mwenyewe na mashataka zinaongelea jambo lingine kabisa na zaidi haziongei kuwepo kwake Oysterbay Police na kuonana na DC Msemwa

Wakili Hilla: Mheshimiwa tuna- submit ya kwamba shahidi ndiye anaye- lay foundation ya upokewaji nyaraka zake bila kufanya hivyo haiwezekani 

Wakili Hilla: Alitakiwa aieleze mahakama ndani ya hizi nyaraka kuna hiki na hiki kinachohusu uandikwaji maelezo ya Ling'wenya au kuhusiana na DC Msemwa

Wakili Hilla: Shahidi anasema alikaa na DC Msemwa, hicho si kigezo cha kuleta nyaraka hizi. nyaraka zilipaswa ziongee zenyewe.

Wakili Hilla: Kwa kifupi Mheshimiwa nyaraka hizi ni irrelevant na shauri hili, hazina sifa.

Wakili Hilla: Kitendo cha kutokuongelea kuwa ni kitu gani kilichomo kinachohusiana na DC Msemwa inaonesha wala hana knowledge ya kile kilichomo.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji nizungumzie sasa charge sheet. Mheshimiwa kinacholetwa mbele yako hakuna ubishi ni photocopy. Hakina ubishi kwa sababu shahidi mwenye alianza kwa kusema huko Kisutu alipewa photocopy.

Wakili Hilla: Rules of evidence zin- demand compliance of procedures ili ulete ushahidi.

Wakili Hilla: Mheshimiwa ni submissions yetu kwamba nyaraka hii imeletwa in violation ya kifungu 63 mpaka 66 ya Evidence Act.

Wakili Hilla: Kwamba kwa kuwa walifahamu kwamba nyaraka ni photocopy walitakiwa Mheshimiwa wa-comply na masharti yanayo-govern utolewaji wa nyaraka hizi.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji baada ya kuwa nimesema hayo naomba mwenzangu Chavula aendelee  atazungumzia hiyo dispatch.

Wakili wa Serikali Abdalah Chavula: Mheshimiwa kama alivyosema mwenzangu nitaanzia alipoishia yeye ambapo ni kwenye hati ya mashtaka ambayo tunasema inakiuka kifungu cha 63 cha Sheria ya Ushahidi.

Wakili Chavula: Ni kweli kifungu cha 63 kinaweza kuthibitisha kwa ama primary evidence au secondary.

Wakili Chavula: Kifungu cha 64 chenyewe kimeweka bayana kuwa primary ni document yenyewe.

Wakili Chavula: Shahidi alisema amepewa photocopy kwa kuwa wakati huo mahakama haikuwa na original. Kwa hiyo ni wazi kwa ushahidi wake hii no copy.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji katika ushahidi wake hajaieleza mahakama kwamba nyaraka hii imekuwa certified.

Wakili Chavula: Shahidi hajaieleza mahakama kwamba nyaraka hii ilitengenezwa kwenye original document na wala hajaiambia mahakama kwamba baada ya kufanyika hayo ilifanyika comparison ili kujiridhisha kwamba kilichomo humu ni sawa na kilichomo kwenye original.

Wakili Chavula: Vilevile hajatoa maelezo ya mdomo kuelezea kilichomo kwenye document hiyo iliyoko mahakamani.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji ni hoja yetu kwamba shahidi huyu wakati wa kuomba kutoa nyraka hii hajakidhi matakwa ya kifungu cha 65.

Wakili Chavula: Vilevile fungu la 67 la Evidence Act, Second evidence inatakiwa itolewe mahakamani.

Wakili Chavula: Ni maoni yetu bila kuchosha mahakama kwa kusoma kifungu baada ya kifungu, maelezo ya kwamba Mahakama ya Kisutu walisema hawana nyaraka nyingine halisi si miongoni mwa vigezo vilivyowekwa kuweza kutoa hii nyaraka.

Wakili Chavula: Ni maoni yetu vigezo katika kifungu cha 65 havijakidhi na chini ya kifungu cha 67 nyaraka hii haitambuliki.

Wakili Chavula: Kwa mazingira haya kwamba wana copy tu walitakiwa waje kwa kifungu cha 68. Kwa kuwa hawaja- exhort hiyo remedy ni maoni yetu kwamba nyaraka hii isipokewe

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji naomba tuelekee kwa pingamizi la dispatch.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji ni msimamo wa Sheria na katika nyakati tofauti tumekuwa tukiielekeza mahakaama kwenye shauri la Charles Abel  Gazilabo na wenzake watatu na nyingine.

Wakili Chavula: Katika kesi hizo mahakama iliweka vigezo kwa shahidi kuweza kutoa vielelezo kwamba kwanza ni ufahamu na awe amekihifadhi

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji kwa hiyo hapa kuna mambo mawili, knowledge na possession.

Wakili Chavula: Ni maoni yetu ili shahidi aaminike na Mahakama yako alitakiwa aende mabali kuonesha ana ufahamu nacho.

Wakili Chavula: Sisi tuna maeneo mawili muhimu.

Wakili Chavula: Wakati anafanya utambuzi wa barua alieleza mahakama kwamba barua ile in reference number. Shahidi hakwenda mbele na kutuambia hiz reference number ni zipi. Ni maoni yetu shahidi alishindwa kunukuu reference numbers za barua ambayo alitoa maelekezo

Wakili Chavula: Kwa kuwa dispatch haitambuliki bila kutaja hizo reference number ni maoni yetu kwamba shahidi hana knowledge na hicho kielelezo.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji kielelezo hiki hakina relevance na kile ambacho kimemleta yeye mahakamani

Wakili Nashon Nkungu anasimama na kupinga: Mheshimiwa Jaji tunaona hiyo ya relevance ni PO (pingamizi) mpya, tunaomba ajikite kwenye PO zilizotajwa mwanzo.

Chavula: Mheshimiwa Jaji tuliambiwa barua hii ilipelekwa mahakamani na afisa wa Tan law, Faith tarehe 13 /11/2020 na yeye alikuja tarehe 24. Lakini hajaieleza mahakama namna Faith alivyomkabidhi barua hii na namna alivyoihifadhi na mpaka anafika hapa kielelezo hicho kilikuwa kimetunzwa wapi na namna gani?

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji naomba kuielekeza mahakama yako shauri la DPP dhidi ya Shrif Mohamed Athuman ambalo tumeshaielekeza.

Wakili John Mallya anasimama nakupinga: Mheshimiwa Jaji naona hiyo ni PO mpya maana kama nilimwelewa msomi Kidando alieleza competence ya shahidi na si kielelezo.

Wakili Chavula: Nadhani amewahi tu nadhani atulie asikilize aone naelekea wapi kama nagusa kielelezo au shahidi.

Jaji: Umesikia unaombwa utulie

Mallya: Sawa, Mheshimiwa natulia, huku akicheka na baadhi ya wasikilizaji wanacheka pia.

Wakili Chavula anaendelea “Mheshimiwa Jaji kielelezo kinatakiwa kioneshe hakikuchezewa”

Wakili Chavula: Hivyo Mheshimiwa Jaji shahidi alipaswa aeleze tangu alipokipata kielelezo hicho mpaka anakuja kukitoa kilikuwa wapi? Kilikuwa katika mazingira ambayo mtu hawezi kujiandikia?

Wakili Chavula: Ni hoja yetu kwamba kukosekana kwa ushahidi huo kwa hayo tuliyoyaeleza kielelezo ama dispatch hii haiwezi kupokelewa.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji namalizia na hati ya mashtaka. Hati ya mashtaka inakinzana na ushahidi wa shahidi. Shahidi anaeleza alikamatwa wilayani Mwanga hati ya mashtaka inaeleza alikamatwa na Makosa yaliyofanywa Dar. Hajaeleza kosa lililofanywa akakamatwa Mwanga na haya yaliyoko kwenye hati.

Wakili Chavula: Hivyo shahidi huyu na vielelezo hivi haziwezi kupokelewa

Wakili Chavula: Ni maoni yetu na ni maombi yetu kwamba katika mazingira haya haviwezi kupokelewa. Ni hayo tu Mheshimiwa.

Upande wa mashtaka umemaliza na sasa ni hoja za upande wa utetezi.

Anasimama wakili wa Nashon Nkungu kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza, Halfan Bwire Hassan.

Kabla ya kuanza, Jaji anamtahadhalisha kuwa kama anaunga mkono basi hapaswi kujielekeza kujibu hoja za upande wa mashtaka.

Wakili wa Serikali Hilla anasimama na kueleza kuwa mawakili wa washtakiwa wengine hawana haki kujibu hoja zao.

Jaji: Nilishalitolea mwongozo na ndio maana nimemsisitiza maana siku hiyo alikuwa na udhuru. Kwa hiyo anaweza kupata uzoefu kwa senior council.

Wakili Nkungu: Bada ya kushauriana kidogo na wakili kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala anaendelea:

Wakili Nkungu: Naunga mkono kupokewa kwa nyaraka hizo zote nne kwa kuwa naona kuwa zimekidhi vigezo. Ameeleza kuzitambua features za nyaraka hizo mfano hati ya mashtaka ametaja namba ya kesi, lakini pia ni relevant kwa kuwa shahidi ameelezea...

Wakili Hilla anasimama na kusema anachokifanya wakili ni kujibu hoja zao.

Wakili Kibatala anasimama na kulalamika kuwa kuna kanuni wameshajiwekea kuwa kutokusimama tu hata bila sababu na kwamba mahakama imeshachukua jukumu la kumuongoza wakili kama atatoka nje na kwamba hata wao hapo wanamnong'oneza.

Wakili Nkungu anaendelea: Naunga mkono pia kwa sababu shahidi ana knowledge. Mahakama ya Rufani imesema tu kuwa shahidi anatakiwa kuwa na knowledge na si sufficient knowlege.

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji nami naunga mkono na nitakuwa kwa ufupi

Wakili John Mallya: Naunga mkono nyaraka hizi kuwa ni relevant na shahidi ameelezea kuwa amewahi kuzimiliki na kile alichokifanya. Nakubaliana na Wakili wa Serikali kuwa nyaraka zinapaswa zijieleze na zikipokewa zitaeleza kilichomo ndani na uhusiano mshtakiwa wa tatu.

Wakili Kibatala: Nasi tunaunga mkono nyaraka hizi kupokewa kwa sababu zimekidhi vigezo. Shahidi ameweka msingi na ameeleza kuwa aliwahi kuzimiliki na aemeeleza uhusiano wake.

Wakili Fredrick Kihwelo, kwa niaba ya mshtakiwa wa tatu (Ling'wenya) ambaye ndio wenye mamlaka ya kujibu hoja za Serikali, anasema kwa upande wao ataanza Wakili mwenzake Dickson Matata.

Matata: Mheshimiwa Jaji nitajibu kwa ujumla na wakili mwenzangu atamalizia. Nianze na suala la relevance. Mheshimiwa Jaji iko kwenye rekodi shahidi jana aliieleza mahakama kwamba alipata taarifa za shahidi SC Msemwa, shahidi wa Jamhuri katika trial within trial.

Matata: Alisema kwamba alipata taarifa kwamba wakati mshtakiwa wa tatu anakamatwa alipelekwa Central Police Dar es Salaam. Shahidi akasema hiyo haikuwa kweli kwa sababu tarehe 14 mwezi wa Tano 2020, baada ya kukamatwa Mwanga na kuletwa Dar es Salaam katika kituo cha Oysterbay alipokelewa na DC Msemwa.

Matata: Hivyo baada ya kupata habari hiyo kwa sababu anajua DC Msemwa alikuwa Oysterbay, alijitolea kuja ku-disapprove alichokisema DC Msemwa.

Matata: Alisema ili kuthibitisha hayo aliwasiliana na wakili wake Peter Kibatala ambaye alishughulika na kesi yake Kisutu, ili aweze kupata charge sheet na proceedings za kesi hiyo.

Matata: Alisema sababu ya kuomba nyaraka hizo ilikuwa ni kuthibitisha kuwa kweli aliwahi kupelekwa polisi Oysterbay na baadaye ndipo akapelekwa Kisutu.

Matata: Ni submission yetu kwamba nyaraka hizi ni relevant kwa sababu malengo yake ni ku-disapprove alichokisema DC Msemwa kwamba. Agosti 7, 2020 alikuwa Central Police Dar wakati yeye shahidi alisema ndipo alikutana naye Oysterbay.

Matata: Kwa hiyo pingamizi la Serikali kwamba nyaraka hizi ni irrelevant sisi tunaona halina mashiko kwa sababu hakuna namna DC Msemwa angeweza kuwa katika vituo viwili tofauti.

Matata: Mheshimiwa Jaji hata bila kuingia kwenye barua yenyewe. Barua ilikuwa inaomba nyaraka hizo ili kuja kuzitumia hapa mahakama.

Matata: Mshemiwa nije kwenye suala la photocopy. Kwamba kwa kuwa ni photocopy hivyo ilihitaji masharti ya kifungu cha 66 cha Sheria ya Ushahidi.

Matata: Mheshimiwa Jaji nianze kwa kusema shahidi alianza kwa ku-lay foundation vizuri kwa kuileza mahakama ni kwa nini amekuja na copy.

Matata: Mheshimiwa Jaji ni submission ya shahidi kwamba yeye mwenyewe akiwa na dada anayeitwa Faith  baada ya kukabidhi  barua hiyo na wakili Kibatala alikwenda Kisutu akiwa na Faith hadi Kisutu hadi kwenye chumba alichokitaja  akamkuta mama ambaye alimpa barua hiyo na baada ya kujiridhisha kuwa inafanana na iliyoko mahakamani, alimpa proceedings na akampa photocopy ya charge.

Matata: Shahidi akamuuliza mimi nimeomba certified kwa nini napewa copy? Yule mama akajibua tumebakiwa na copy moja.

Jaji: Mimi nimerekodi " hii ndiyo tuliyonayo"

Matata: Sawa Mheshimiwa Jaji. Sasa Mheshimiwa jaji fault ya kupewa copy si yake ni ya Mahakama na Mahakama ilitoa sababu kwa nini ilimpa photocopy.

Matata: Hivyo ni submission yetu Mheshimiwa Jaji kwamba sisi tunaona pingamizi hili halina mashiko kwa sababu kifungu cha 67(c) Sheria ya Ushahidi kinaruhusu kutumia copy kwenye mazingira kama haya ya kesi hii.

Matata: Mheshimiwa Jaji kifungu hiki kinaruhusu kutumika kwa photocopy pale ambapo mtu anayetakiwa ameshindwa kupata original si kwa sababu ya uzembe wake au makosa yake.

Jaji: kifungu kinazungumza kutumia photocopy au secondary evidence?

Matata: Second evidence.

Matata: Tulipaswa kuleta maombi chini ya kifungu cha 68 lakini ili hiki kiweze kutumima ni lazima mashart yaliyoko katika kifungu cha 67(1)(c).

Matata: Ni rai yetu kifungu hiki kinaweza kutumika na hatuja offend Kanuni zozote.

Matata: Kwa kuzingatia kwamba photocopy hii alipewa na Mahakama, ni submission yetu kwamba kwa kifungu cha 68(g) Sheria ya Ushahidi

Matata: Mahakama inaweza kukipokea kifungu hiki hasa kwa kuzingatia kwamba tumekileta kwa wakati. Hivyo pingamizi hili halina mashiko.

Mheshimiwa Jaji nipo kwenye suala la competence na hasa ya dispatch.

Matata: Shahidi alisema alipokuja Dar es Salaam alipewa dispatch akaenda mahakama ya Kisutu akiwa na Faith

Wakili wa Serikali Hilla anasimama na kupinga: Mheshimiwa naomba Wakili asizungumze  maneno ambayo hayapo. Mfano hakuna mahali shahidi alisema alipewa dispatch na Wakili Kibatala, alisema alimuunganisha na mtu mwingine aitwaye Faith. Kwa hiyo kama wakili anaamua kutumia maneno ya shahidi atumie maneno aliyoyatamka.

Matata: Mheshimiwa Jaji, Mimi nakumbuka alisema hivyo.

Jaji anarejea kwenye Kumbukumbu za mahakama kuhusu ushahidi wa shahidi. Hata hivyo Hakuna mahali kwamba alikabidhiwa dispatch.

Jaji: Tukakubaliana kwamba kumbukumbu za ushahidi zinasema kuwa shahidi alisema kuwa mpaka anakuja hapa mahakama alikuwa nazo nyarka hizo tangu alipopewa.

Wakili Hilla: Ni sawa Mheshimiwa lakini tunachopinga ni kwamba hakuna mahali amesema alikabidhiwa lini hiyo dispatch.

Jaji: Ndio ni sawa.

Wakili Matata anaendelea: Lakini pia shahidi alieleza kuwa tangu alipopewa nyaraka hizo, barua, dispatch, proceedings na chargesheet yeye ndo aliendelea kuzitunza.

Matata: Alionesha kuwa na knowledge anayo. Alitaja feature mbalimbali ikiwemo rangi ya pinki ya dispatch, pia juu yake kuna neno Court 2 na maneno yaliyosomeka classic na ndani ya hiyo dispatch kuna anuani ya Mahakama ya Kisutu.

Matata: Kwa hiyo ni rai yetu kwamba shahidi huyu ni competent na hoja ya pingamizi ni competence na si chain of custody.

Matata: Kwa hiyo tunaomba mahakama inapotoa uamuzi ijielekeze kwa kile kilichoamuriwa na Mahakama ya Rufani katika rufaa ya Jinai  Namba 463 ya mwaka2016, kuwa possessor anaweza ku- tender exhibit.

Matata: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji kwa sababu shahidi alionesha kuwa ana knowledge na document kwa sababu alii-possess.


Advertisement