Kina Mbowe wakwama mahakamani

Monday November 29 2021
mbowepic
By James Magai

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imekubali pingamizi la mawakili wa Serikali la kutopokea barua kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya ugaidi inayomkabili Mwenyeki wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Novemba 29, 2021 na Jaji Joachim Tiganga na kueleza kuwa mshtakiwa huyo Mohamed Ling'wenya hajaweza kuieleza mahakama ni kwa nini barua hiyo inamhuri wa naibu msajili.

SOMA ZAIDI: Kinachosubiriwa kesi ya kina Mbowe leo

Jaji ameeleza kuwa katika mazingira hayo mahakama imeshindwa kuelewa kama hiyo barua aliyotaka kuitoa ndio hiyo iliyopelekwa kwa RPC.


Fuatilia hapa uamuzi ulivyotolewa na Joachim Tiganga;

Advertisement


Jaji Tiganga ameingia na kesi inaitwa na karani

Mawakili wa Serikali wanatambulishwa na kiongozi wa jopo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando

Mawakili wa utetezi saa wanatambulishwa na kiongozi wa jopo, Peter Kibatala.

Jaji anawaita washtakiwa mmoja mmoja kwa namba nao wanaitika

Wakili wa Serikali Kidando: Mheshimuwa Jaii shauri hili linakuja kwa ajili ya ruling, na tuko tayari

Kibatala: Na sisi Mheshimiwa Jaji tuko tayari kupokea ruling pamoja na kuendelea kadri Mahakama itakavuoelekeza

Jaji Tiganga: Mahakama imeandaa maamuzi na haya ndio maamuzi yenyewe. Kwa kuwa maamuz ni marefu nitasoma maeneo muhimu lakini hoja zote zimezingatiwa.

Sasa Jaji Tiganga anaanza kusoma uamuzi kwanza akifanya muhtasari wa chimbuko la pingamizi na hoja za pande zote, kabla ya kufanya uchambuzi wake na hatimaye kutoa hitimisho kama pingamizi linakubaliwa au linatupiliwa mbali.

Jaji Tiganga: Kuhusjana na unique feature za kielelezo (barua) mahamama imeridhika kuwa shahidi (mshtakiwa) ameweza kuzitaja ambazo ni uwepo wa sahihi ya wakili, jina lake shahidi (mshtakiwa) na mhuri wa Mahakama. Hivyo mahakama imetupiliabmbali hoja ya kwanza ya pingamizi

Sasa Jaji Tiganga anajadili hoja ya pili: Pingamizi la Serikali linalohusu Chain of custody (mnyororo wa uhofadhi wa kielelezo).

Shahidi hajaweza kueleza akioneshwa. Na wakili wake barua hiyo wapi na lini na ni muda gani ameweza kuutumia kuwa na uelewa na kielelezo hicho na kwamba amekutana nacho katika mazingira gani mpaka aweze kukitoa mahakamani.

Mahakama ya Rufani ilishaweka wazi kuwa moja ya kigezo shahidi kutoa kielelezo ni kuwa na uelewa kuhusiana na kielelezo hicho.

Katika haki hiyo na kubakiana na upande wa Jamhuri kuwa shahidi alitakiwa aonyeshe kuwa ana uelewa wa kielelezo na alitakuwa alifanye hilo wakati akitoa ushahidi.

Kuonyeshwa tu kielelezo bila ushahidi kuwa amekimiliki ni jambo ambalo haliko kisheria.

Pia hajaeleza baada ya kuoneshwa kielelezo hicho alikifanyia nini kama aliona content.

Hivyo mahakama inashindwa kuamini kuwa shahidi huyu ana uelewa wa kielelezo hicho

Lakini pia katika eneo hilo barua hiyo imeelekezwa kwa Kamanda wa Polisi Ilala na nakala kwa mshtakiwa na kwa Naibu Msajili.

Ni kweli nyaraka iluyoombwa kutolewa hapa mahakamani ni barua iliyoandikwa kwa Kamanda wa Polisi Ilala.

Nakubaliana shahisldi akipewa nakala na pale mtoa nyaraka anapotoa nakala kwa mtu mwingine anakuwa analenga kuwa imfikie.

Hata hivyo kuna kigezo na moja lazima huyo aliyepewa aseme aliipokea na lazima atoe hiyo aliyopewa.

Lakini nyaraka aliyooneshwa shahidi tayari ilikuwa na mhuri wa Msajili, katika mazingira hayo nakala anayotaka kuitoa si nakala yake maana yake isingekuwa na mhuri bali anataka kutoa nakala iliyopelekwa kwa Msajili.

Shahidi hajasema ilikuwaje ikamfikia yeye.

Hivyo shahidi hajaweza kuiambia mahakama ni kwa nini barua anayotaka kuitoa ina mhuri wa Naibu Msajili.

Katika mazingira hayo mahakama inashindwa kuelewa kama hii anayotaka kuitoa ndio hiyo iliyopelekwa kwa RPC

Katika mazingira hayo mahakama inaona shahidi ameshindwa kuthibitisha chain of custody hivyo inakikataa kielelezo hicho.

Baada ya uamuzi huo sasa shahidi huyo wa kwanza wa utetezi katika kesi ndogo (mshtakiw Ling'wenya) anaendelea na ushahidi wake.

Kwanza Jaji anamkumbusha shahidi kuwa bado yuko chini ya kiapo.

Kisha Wakili wake Dickson anaendelea kumuongoza kutoa ushahidi wake.

Shahidi: Mimi Central Dar sijafika ndio maana nikamuomba Kamanda kuwa aweze kutoa uthibitisho kuwa shahidi huyo (wa pili upande wa mashtaka) alinipokea Central tarehe 7, 2020 maana mimi tarehe hiyo 7, 8 na 9 nilikuwa kituo cha Polisi Tazara

Kwenye ile selo niliyokuwepo (Tazara) kulikuwa na mahabusu wengi na sikupata muda wa kuingia kuongea nao.

Wakili Matata: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Shahid amemaliz ushahidi wake wa msingi na sasa anahojiwa na kwanza mawakili wa washtakiwa wengine kisha watafuata upande wa mashtaka.

Anaanza wakili wa mshtakiwa wa kwanza (Halfan Bwire) wakili Nashon Nkungu:

Wakili: Ulisema ulikuwa inachukuliwa video, nani alikuwa anakuchukua video?

Shahidi: Nilichukukuwa video Moshi na Tazara, aliyenichukua Moshi ni tofauti na wa Tazara ambaye simfahamu.

Wakili: Ni wakati wa tukio gani ulikuwa unachukuliwa video?

Shahidi: Moshi ilikuwa wakati napigwa na Tazara wakati nahojiwa

Wakili: Unafahamu kwamba ni takwa la kisheria ukihojiwa kuchukuliwa video?

Shahidi: Nimekuja kujulia hapa Mahakamani

Wakili: Umeziona hapa mahakamani hizo video zikitolewa?

Shahidi: Hapana sikuziona

Wakili: Unafahamu ni takwa la kisheria mtuhumiwa kufikishwa mahakamani mara moja?

Shahidi: Nafahamu

Wakili: Unafahamu mara kadhaa DPP ametoa mwongozo mtu asifikishwe mahakamani mpaka upelelezi ukamilike?

Shahidi: Ndio Nafahamu

Wakili: Wewe ulikamatwa lini?

 Shahidi: Tarehe 5/8 /2020

Wakili: Ulifikishwa lini Mahakamani kwa mara ya kwanza?

Shahidi: Tarehe 19/8/2020

Wakili: Iliikuwa ni baada ya siku ngapi?

Shahidi: Siku 14

Wakili John Mallya: Ulipokamatwa Moshi cha kwanza kufanyiwa ni ninj?

Shahidi: Nilipelekwa kwenye chumba cha mateso

Wakili: Ni kitu gani shahidi uhijisi ni chumba cha mateso?

Shahidi: Nilikutana na rungu, chuma na kamba.

Wakili: Ulikuwa katika hali gani?

Shahidi: Nilikuwa nimefungwa pingu mikono, ile kamba nikafungwa miguu, bomba kikapitishwa katikati ya miguu na mikono wakainua

Wakili: Ukawa katika hali gani wakati huo?

Shahidi: Nikawa kama popo naning'inia

Wakili: Watu gani hao wakihusika kukufanya uning'inie?

Shahidi: Upande mmoja alishika Jumanne, upande mwingine Goodluck na Mahita ndio alikuwa ananipiga na rungu

Wakili: Mahita alikupiga sehemu gani?

Shahidi: Wakati huo Kingai alikuwa wapi?

Shahidi: Yeye alikuwa amesima a tu pembeni

Wakili: Hilo zoezi la kukupiga kwenye nyayo lilichukua mudu gani?

Shahidi: Lilichukua kama nusu saa

Wakili: Walikuwa wanakuuliza nini?

Shahidi: Kwamba umekuja kufanya nini Moshi?

Wakili: Uliwajibuje?

Shahidi: Kwamba nimekuja kwa ajili ya VIP Protection kwa Mheeshimiwa Mbowe, wao walikuwa wanakataa kwamba sisi tunajua tulichokuja kufanya

Wakili: Nani alikuwa anauliza?

Shahidi: Alikuwa anauliza mmoja lakini wengine wanadakia kuwa siyo kweli, sisi tunajua

Wakili: Baadye kilitokea nini?

Shahidi: Nilisikia sauti ya mtu kuwa muacheni

Shahidi: Ilikuwa ya nani?

Shahidi: Sijui lakini kama alikuwa askari

Wakili: Nini kilifuata?

Shahidi: Nilifunguliwa nikarudishwa mahabusu

Wakili: Lini ulifunguliwa pingu?

Shahidi: Nilifunguliwa pingu tarehe 19/8/2020 mahakamani Kisutu

Wakili: Kuna watu wengi hapa wamekuja wakasema baada ya kukamatwa mlikwenda sijui kuwatafuta watu gani?

Shahidi: Ni uwongo

Wakili: Kuna huduma gani za kijamii?

Shahidi: Pale Moshi mimi sikupewa chakula

Wakili: Sasa nakuja safari ya Dar, nani alikutoa mahabusu?

Shahidi: Goodluck na Mahita.

Wakili: Ulikuwa katika hali gani?

Shahidi: Nilikuwa nimeinamishwa shingo, baadaye nikamuona Adamoo naye analetwa, akaingizwa kwenye gari kisha nikafungwa kitambaa kizito usoni.

Wakili: Lengo lao lilikuwa nini?

Shahidi: Labda walitaka nisione napelekwa wapi.

Wakili: Mikono ilikuwa katika hali gani?

Shahidi: Ilikuwa imefungwa pingu

Wakili: Safari yako ilikuwaje? Luxury au ya namna gani?

Shahidi: Ilikuwa ya mateso maana nilikuwa nimeinamishwa tu shingo na kufungwa kitambaa.

Wakili: Ni nini kilikufanya uone ni mateso?

Shahidi: Kulingana na vitendo nilivyokuwa nafanyiwa

Wakili: Mliondoka saa ngapi?

Shahidi: Jioni na tukafika alfajiri Dar

Wakili: Kwa masaa hayo uliyokuwa njiani kuna huduma yoyote ya kibinadamu ulipata?

Shahidi: Hakuna huduma ya kibinadamu nilipata

Wakili: Chakula?

Shahidi: Sikupata chakula hadi waliponifikisha Tazara

Wakill: Wale wasafirishaji wako walikwambia ni Tazara?

Shahidi: Hapana, mlango ulifunguliwa tu nikashushwa nikiwa nimefungwa kitambaa, nikaingizwa selo

Wakili: Kilichokusaidia kujua mlango umefungululiwa ni nini?

Shahidi: Nilisikia tu kwa masikio

Wakili: Pale Tazara kutuoni kuna mahali uliandikishwa?

Shahidi: Mimi sikuandikishwa popote nilipitishwa tu mpaka mahabusu

Wakili: Mikono ilikuwaje?

Shahidi: Ilikuwa bado imefungwa pingu

Wakili: Ulisema baadaye ulihamishiwa kituo cha Mbweni, hali ilikuwaje?

Shahidi: Bado nilikuwa nimefungwa pingu na kitambaa.

Wakili: Njiani ilikuwaje?

Shahidi: Nilikuwa natishwa kwamba ukicheza tutakupoteza kama Lujenge kule Moshi, halafu Goodluck alikuwa ananichomachoma kwenye mbavu na kitu kama bastola

Wakili: Kwa nini ulihisi ni bastola?

Shahidi: Maana Goodluck muda mwingi alikuwa ameshika bastola.

Wakili: Ulisema baadaye akaja Jumanne na maelezo akakulazimisha kusaini, ulikuwa katika hali gani?

Shahidi: Niliogopa maana Goodluck alikuwa amesimama mlangoni na bastola anakasema ukileta janjajanja tutakufanya kama Moshi.

Wakili: Nilikusikia ukiwataka wanajeshi wengine hapa, hao ushiriki wao ukikuwaje katika hili?

Shahidi: Nlikutana nao tu kwa mara ya kwanza Tazara wakaniambia usihofu hapa ni Tazara sasa labda walitaka kuhakikisha kuwa na mimi nimetoka JWTZ

Sasa ni zamu ya mawakili wa Serikali anaanza wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla

Wakili wa Serikali (WS): Shahidi, ni mara yako ya ngapi kutoa ushahidi?

Shahidi: Ni mara ya pili

Jaji Tiganga: Muongeze sauti nami niweze kusikia nawe (wakili) ugeukie huku.

Kesi imeahirishwa kwa dakika 10 baada ya shahidi (mshtakiwa) kupitia wakili wake Matata kuwa anataka kwenda short call, Jaji akitoa nafasi na kwa wengine wanaohitaji kupata huduma hiyo.

Mahakama imerejea na upande wa mashtaka unaendele kumhoji shahidi

Wakili Hilla: Dada yako yuko Moshi kwa muda gani?

Shahidi: Miaka mitatu inaweza kufika

WS: Shahidi ni sahihi tarehe 4/8/2029 ulikuwa Moshi?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi tarehe 5 ulikuwepo Moshi na ulikamatwa na kina Kingai, Jumanne na Mahita?

Shahidi; Ni sahihi


WS: Ni sahihi kwamba hao watu, Kingai na wenzake wakati unajitetea hujaieleza mahakama mlikuwa mnafahmiana?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi kwamba hujaieleza Mahakama kama ulikuwa na ugomvi nao?

Shahidi: Ni sahihi


WS: Bwana Ling'wenya, ulikamatwa saa ngapi?

Shahidi: Saa 7 Mchana

WS: Ni sahihi kama walivyosema kina Kingai?

Shahidi: Ni sahihi?WS: Ni sahihi wakati mnakamatwa watu walishuhudia?

Shahidi: Ni sahihi maana ilikua sehemu ya wazi

WS: Ni sahihi kwamba mlikuwa na Moses Lujenge ambaye alitoroka?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Bwana Ling'wenya ni sahihi ya kwamba hujaionesha mahakama eneo la mwili wako unakodai ulipigwa?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Na ni sahihi ya kwamba neno kupigwa kwenye unyayo, kina Kingai, kina Majita na Jumanne walipokuja hapa hukuwauliza badala yake umelisema leo?

Shahidi: Kimya

WS: Bwwna Ling'wenya....

Wakili Matata anapinga swali hilo akiungwa mkono na wakili Mallya na Kibatala wakieleza kuwa mahakama ilishatoa angalizo kuwa makini ili mwenendo wa kesi ndogo usiingilie kesi ya msingiWakili Matata anafafanua kuwa kina Kingai na Mahita hawajaja kutoa ushahidi kwenye kesi hii ndogo na Jaji anakubaliana na hoja anamtaka wakili Hilla arekebishe swali.

WS: Shahidi ni sahihi mashadi waliokuja hapa hukuwauliza kuhusu kupigwa kwenye nyanyo?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Kina Jumanne na Goodkuck walikuja hapa na hukuwauliza kuhusu kunyanyuliwa kwenye bomba?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi hujaleta hapa barua ya kitabibu kuthibitisha kupigwa kwako na kupata majeraha?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi kwamba jujawahi kumwandikia barua mtu yeyote malalamiko yako haya ya kupigwa?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi hata ulipofikishwa mahakamani hukumwambia hakimu kuwa ulipigiwa?

Shahidi: Si sahihi

WS: Si sahihi kwa sababu ulisema kwenye commital?

Shahidi: Hakimu Simba nilishamwambia na kumlalamikia yote yaliyotokea

WS: Kumbukumbu za mahakama ulishazisoma kabla ya commital?

Shahidi: Hapana

WS: Uliwahi kuandika barua kulamika kuwa hakuandika malalamiko yako?

Shahidi: Hapana

WS: Shahidi, unataka mahakama ikuamini kuwa ulikuwa unajisaidia na pingu mikononi?

Shahidi: Ndio

WS: Na unataka mahakama ikuamini kuwa ulikuwa unakula na pingu mikononi?

Shahidi: Kula wapi?

WS: Mahabusu, si ulisema ulikuwa unakula bisukuti?

Shahidi: Mimi nimeshaieleza mahakama kuwa nilikuwa na pingu muda wote mpaka tarehe 19. Sasa unataka mimi nijibu tu masuala yote ya kujisaidia, kula nijibu tu?

WS: Ulisema kuwa Central Moshi ulifikishwa kwenye chumba cha mateso, uliwahi kulalamika kwamba Central kuna chumba cha mateso?

Shahidi: Hii si mara ya kwanza nilishasema...

WS: Nakuuliza ulishawahi kulalamika popote kuwa Central Moshi kuna chumba ha mateso?

Shahidi: Nilishawahi kusema hapa kuwa niliteswa...

WS: Nakuuliza ulishawahi kulalamika?

Shahidi: Sijawahi

Wakili Matata: Obejrction Mheshimiwa Jaji shahidi ameshajibu swali

Jaji: swali lako limeshajibiwa (WS)

WS: Bado

Jaji: Hebu uliza

WS: Labda nikuulize hivi ulishawahi kulalamika kwa maandishi kuwa Central kuna chumba cha mateso?

Shahidi: Kwa maandishi sijawahi

WS: Ulisema Central Moshi ulirekodiwa video ukiteswa?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi hujamtaja hata jina aliyekurekodi?

Shahidi: Sikumuona

WS: Unajua kwamba kuna sheria inayohueu kurekodi video?

Shahidi: Sijui

WS: Na unajua kwamba kuna mazingira maalumu ya kurekodi video?

Shahidi: Sijui

WS: Ni sahihi kutoka Moshi ulisafiriashwa na Jumanne, Goodluck na Mahita?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Kwa hiyo waliokusafirisha ulishawaona ulishawajua?

Shahidi: Ndio?

WS: Ni sahihi stori, ushahidi wako unafanana na kina Kingai kwamba ulisafirisha kutoka Moshi tarehe 6/8/2020

Shahidi: Kwa kumbukumbu zangu ni tarehe hiyo.

WS: Ni sahihi kwamba Moshi mlikuwa na Lujenge kwa ajili ya kuonana na Mbowe?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando.

WS: Ulifuatilia trial within trial ya Adamu wakati mnaondoka Moshi ilikuwa ni mchana, Ni sahihi?

Shahidi: Kimya

WS: Lakini ushahidi uliondoka na kina Jumanne na mlifika Dar tarehe 7/8/2020 alfajiri, ni sahihi?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Kama nilikusikia wakati ukiulizwa na Kibatala, vituo vya Central Dar, Tazara na Mbweni ulikuwa huvijui?

Shahidi: Ndio ni sahihi

WS: Ni kitu gani kiikufanamisha kuwa baada ya kukamatwa mlipelekwa Central Moshi?

Shahidi: Wakati huo tilikuwa hatujafungwa kitambaa

WS: Wakati mnakamatwa Dada yako Asmah alikuwapo?

Shahidi: Pale sikumuona lakini ni karibu tu na dukani kwake lakini kulikuwa na watu wengi sasa sijui kama alikuwepo.

WS: Je, unajua kuwa yeye alitoa taarifa wapi?

Shahidi: Yeye ndiye aliyesimamia taarifa kwamba sisi tumeletwa Dar.

WS: Utakubaliana nami kwamba kwa mara ya kwanza sula la Goodluck na Jumanne kukushikilia bomba uliutoa kwa mara ya kwanza wakati unahojiwa na wakili Mallya?

Shahidi: Kwa majina kuwata, ndio ni sahihi.

WS: Na ni kweli kwamba Jumanne na Goodluck walipotoa ushahidi kwenye kesi hii hawakuulizwa swali kwamba wao ndio wakishikilia bomba?

Shahidi: Kwa kumbukumbu zangu waliulizwa kwamba wao ndio walikuwa wananitesa

WS: Sikiliza swali langu, nakuilizwa kuhusu swali kwamba wao ndio waliokuwa wamesHikilia bomba, kama hukumbuki sema tu tuendelee

Shahidi: Ni sahihi

WS: Ni sahihi kwamba wakati unatoa ushahidi wako ukiongozwa na Matata, hukuwataja?

Shahidi: Ni sahihi sikuwataja

WS: Unakumbuka wakati unatoa ushahidi wako Alex Ahadi na Chuma Chunguru kwenye kesi ndogo ukimtetea Adamu Kasekwa hukusema kuwa ulikutana na wadepo wako iliyopelekwa ghorofani Tazara?

Shahidi: Nilisema na nikawataja...

WS: Sikiliza swali langu, ulisema ulikutana nao ghorofani?

Shahidi: Sikusema

WS: Wakati shahidi wa nne, Mkuu wa kituo cha Tazara akitoa ushahidi wake hapa ulimsikiliza?

Shahidi: Ndio

WS: Na kwa maelekezo yako kwa wakili Matata DR ilipokewe bila kupingwa?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Kwa Sasa una ufahamu kuhusu matumizi ya DR?

Shahidi: Nimepata uelewa kidogo

WS: Kuna mahali mahabusu anatakiwa kuandika kwa mkono?

Shahidi: Hilo sielewi vizuri

WS: Umesema hapa wakati uko polisi Tazara, kama ni kweli ulikuwa unarekodiwa video ukitoa maelezo yako?

Shahidi: Ni sahihi

WS: Lakini hujasema ulikuwa unaulizwa nini?

Shahidi: Nilisema nikikuwa naulizwa particular zangu na kuhusu Moshi.

WS: Nimesema Tazara, siyo Moshi

Shahidi: Sijasema

WS: Sasa yale makaratasi unayosema alikupa Jumanne ulisaini?

Shahidi: Sikusaini, nililazimiashwa

WS: Lakini hatimaye ulisaini hukusaini?

Shahidi: Nilisaini

WS: Ulisainije kwa dolegumba au ulisainije?

Shahidi: Siikumbuki nilisainije

WS: Na kwenye ushahidi wako hujasema kama ulisaini ukiwa na pingu au ulifunguliwa?

Shahidi: Nilikuwa na pingu

WS: Lakini hujasema?

Shahidi: Kimya

WS: Unakumbuka pale Kisutu, siku ya commital malalamiko yako uliyoyatoa?

Shahidi: Nakumbuka nilisema kuwa sikuyasoma

WS: Na siku hiyo katika malalamiko uliyoyatoa hukumtaja SP Jumanne?

Shahidi: Sikumbuki

WS: Kuhusu Goodluck?

Shahidi: Sikumbuki

WS: Na Wala siku hiyo haukulalamikia kuwa ulipata vitisho vya kisaikolojia?

Shahidi: Nilisema kuwa nilipata vitisho.

WS: Mhhu: Kuhusu vitisho vya kisaikolojia

Shahidi: Sikumbuki

WS: Ni nani aliyatoa malalamiko hayo?

Shahidi: Ni mimi mwenyewe

WS: Na Unafahamu mpaka tunafika shauri dogo na mapingamizi yote hakuna pingamizi uliloleta kwamba uliteswa Dar?

Shahidi: Sijaelewa

WS: Nakuuliza katika malalamiko yako kuna sehemu umelalamikia kuwa umeteswa jibu swali maana yameshaandikwa

Shahidi: Nilisema niliteswa si nilishatishiwa?

WS: Kwa ufahamu wako vitisho vya kisaikolojia unafahamu?

Shahidi: Labda kwa mifano

WS: Jibu swali unafaamu?

Shahidi:  Ni kama hofu

WS: Hapa Mahakamani ulitoa ushahidi kuwa ulimweleza wakili wako baada ya shahidi wa pili kwamba afuatilie mambo fulani barua ile mpaka leo hujapatiwa majibu,

Shahidi: Nilimuelekeza

WS. Na hukutoa ushahidi hapa mahakamani kama barua ile ilimfikia RPC Ilala?

Shahidi: Sijaema

WS: Wala hujaeleza nani aliipeleka?

Shahidi. Sijasema

WS: Wala hujasema mambo yaliyomo ambayo yalikuvanya uitambue.

Jaji: Hiyo barua haiko kwenye kumbukumbu sijui kwa nini unataka kuiingiza

WS: Ulisema Mbweni ulipewa karatasi kwamba sasa jina lako ni Johnson John hujakileta hapa mahakamani?

Shahidi: Sijakileta

WS: Wala hujaeleza kama ulikuwa na tuhuma nyingine mpaka ukapewa hilo jina?

Shahidi: Ndio sijasema

Wakili Kidando amemaliza sasa ni Abdsllah Chavula.

Wakili Kidando amemaliza sasa ni Abdsllah Chavula.

Chavula: Kama Nilikisikia vyema, ulieleza vyema ile Committal uliisoma na kuridhika Ni kweli au sio kweli?

Shahidi: Nisahihi 

Chavula: Samahani Jaji nataka nirejee kwenye kumbukumbu za Mahakama ya Kisutu.

Chavula: Shahidi 23/8/2020 mlikiwa Mahakama ya Kisutu, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba mkasomea ushahidi unaotarajia kutolewa na upande wa mashtaka katika kesi yenu?

Shahidi: Sina kumbukumbu vzr.

Chavula: Na kweli mlipewa nafasi ya kusikiliza malalamo yenu? Na hapa mahakamani hujawahi kutoa makaratasi yoyote uliyopewa na kusaini?

Shahidi: Ni sahihi.

Chavula: Ni sahihi mbele ya Hakimu Simba kule katika Mahakama ya Kisutu, ulitoa maelezo yako na kuandikwa lakini hukupewa kuyasoma? Sasa iweke wazi mahakaka kati ya maeelezo uliyoyasema Kisutu na haya uliyoyasema Mahakama hii yapi Ni sahihi?

Shahidi: Kimya

Wakati Chavula anaendelea kumhoji shahidi( Ling'wenya), Wakili Nashoni Nkungu amesimama na kueleza Mahakama kuwa Chavula anakiwa kuhoji shahidi kutokana na ushahidi alioutoa katika records.

Shahidi amejibu swali kuhusu Mahakama ichukue lipi iache lipi?

Shahidi: Nilikiri kutoa maelezo huku nikiwa nimeteswa.

Chavula: 8/8/2020 kwa madai yako ulivyokuwa pale Tazara, ulitembelewa na watu gani?

Shahidi-Huko Tazara sikutembelewa.

Chavula- Hukuona watu waliokuja kukuona?

Shahidi- Walikuwepo askari ambao nilifanya nao kazi pale kikosi 92KJ.

Shahidi- Nilimuona Alex Ahadi na Chuma Chunguli.

WS: Ukiacha Alex na Chuma Chuguli nani mwingine ulimuona?

Shahidi- Kingai, Jumanne na Mahita.

WS- 9/8/2020 ulimuona nani na nani?

Shahidi-Nilimuona Chuma Chungulu, Goodluck na Alex anaongea na simu na Denis Urio, niliwaona baada ya kuchungulia kwenye tundu.

Chavula- Wakati unatoa ushahidi wako kwa mara ya kwanza hukumtaja kama siku hiyo alikuwepo Goodluck, sasa  kati ya ushahidi wa awali na huu wa sasa Mahakama ibebe upi?

Shahidi- Nilishaeleza.


Chaula: Shahidi tuambie kuanzia 5/8/2020 hadi 19/8/2020, ulikaa siku ngapi bila kula chakula?

Shahidi: Niliieleza mahakama kuwa sikuwa napata ratio za mahabusi, Nilisema kuna askari mmoja alikuwa ananiletea biskuti na maji.

Jaji: Sikiliza swali

Shahidi: Tazara nilikula ugali na mboga za majani.

Shahidi: Nilikaa siku 12 bila kula chakula.

Chavula:Kwa hiyo shahidi ni umekaa siku hizo bila kula chakula.

Shahidi: Ni kwa ration ya mahabusu ndio chakula cha mahabusu sikupata.

Chavula: Tazara ulifika tarehe ngapi?

Shahidi: Agosti 7, 2020 na kuondoka Agosti 8, 2020.

Chavula: Shahidi tueleze Askari aliyekuwa anakuletea hizo Biskuti.

Shahidi: jina Simfahamu Ila nilisoma cheo chake ni Coplo.

Chavula: Ni sahihi hukuieleza.mahakaka biskuti alizokuwa anakuletea zilikuwa na wingi kiasi gani?

Shahidi: Nisahihi

Chavula: Ni sahihi hukueleza mahakama Askari huyo alikuwa anakuletea Mara ngapi biskuti hizo?

Shahidi: Ni sahihi Sijaiambia Mahakama.


Chavula: Ni sahihi hukuiambia mahakama, Askari huyo alikuwa anakuletea bisktuti Mara ngapi kwa siku?

Shahidi: Alikuwa analeta biskuti kila aliingia.

Chavula: Ile DR ya Tazara haijasema hata mara moja, Ni sahihi wewe hujawahi kuandikwa katika kituo hicho?

Shahidi- Ni sahihi.

Chavula: Ni sahihi DR ya Central Polisi Dsm, ina majina yako?

Shahidi- Nisahihi

Chavula: Sasa iambie mahakaka kati ya Adamu aliyedai alitolewa kituo cha Polisi Mbweni Agosti 9 na wewe unasema ulitolewa kituo hicho Agosti 10, 2020, sasa mahakaka ichukue lipi?

Shahidi- Sikumbuki.

Chavula: Sasa kama kumbukumbu za Mahakama zikionyesha kuwa ilikuwa Agosti 10, 2020 itakuwaje?

Shahidi- Siijui

Chavula- Shahidi ni sahihi, siku ya Agosti 10, 2020 ulikutana na Denis Urio? Ni Sahihi

Shahidi- Ndio nilimuona Denis Urio kwenye korido.

Chaula: Swala langu, katika ushahidi wako wa awali, hukusema kuwa Denis Urio ulipishana pale Mbweni kituo Cha Polisi? Ni Sahihi

Shahidi- Ni sahihi.
Chavula: hebu mueleze chumba alichokuwa anatokea Adam kilo upande gani? Hebu elezea hapo ulipokaa ...tuambia chumba alichotokea Adamu kilikuwa upande gani?

Shahidi: Kilikuwa nyuma yangu hapa nilipokaa.

Chavula: Chumba hicho kilikuwa nyuma kwenye mlango? Ni sahihi

Shahidi: Nisahihi

Chavula: Na Goodluck alikuwa amesimama kwenye mlango wa chumba Cha Adamu, je ni sahihi wewe ulipokuwa umekaa kwenye chumba pale kituo Cha Mbweni, Goodluck ulikuwa umempa kidogo?

Shahidi: Ni sahihi.

Chavula: Ahhh kwani shahidi ulishawahi kueieleza Mahakama kwenye ushahidi wako wa awali, ulikuwa umekaa upande gani?

Shahidi: Kimya.

Chavula: Shahidi Unafahamu inspekta Maulidi?

Shahidi: Nafahamu

Chavula: Ni sahihi wewe hukuwahi kuleta swali juu ya sajent Kidume, hadi leo?

Shahidi- Ni sahihi.

Chavula: Mheshimiwa Jaji Sina swali lingine kwa leo.

Jaji: Tunabreak kwa muda wa nusu saa huu hadi saa 9:00 mchana tukapoendelea.

Jaji ameshaingia mahakamani na pande zote wanajitambulisha

Kwa sasa shahidi anaongozwa na wakili wake, Dickson Matata kujibu baadhi ya maswali ambayo alihojiwa na mawakili wa upande wa mashtaka.

Matata: Shahidi uliulizwa na mawakili wa upande wa mashtaka kuwa huonyesha makavu yaliyotokana na pingu, hebu ifafanulie Mahakama kwanini hukuonyaonyesha hapa mahakamani?

Shahidi: Sijaonunyesha kwa sababu saiizi ni mwaka sasa umepita.

Matata: Uliulizwa maswali mengi kuhusiana na wewe kufikishwa kituo cha Tazara, je ieleze kwanini kuhusema?

Shahidi: Sikusema kwa sababu wao walikuwa wanazungumzia kesi ndogo kuhusiana Adamoo

Matata: Uliulizwa kuhusiana na Mbweni, hasa suala la pingi, na chakula, sasa ifafanulia mahakaka kuhusiana na pingu.

Shahidi: Nilisema Mbweni sijawahi kufunguliwa pingu na kuhusu chakula nilikuwa nasaidia na Askari kwa kuletewa biskuti.

Wakili wa Serikali Robert Kidando amenyanyuka na kueleza mahakama kuwa baadhi maswali ya wakili Matata anayemuongoza shahidi huyo, hakuyasema hivyo anamuomba ajikite kwenye maswali ambayo upande wa mashtaka walimhoji shahidi, Mheshimiwa Jaji sisi hatujamuuliza shahidi swali lolote ambalo jibu lake alijibu mkate.

Jaji: Mimi Sijamsikia shahidi akisema alipewa mkate na hapa kwenye kumbukumbu sijandika mkate.

Matata: Namemmuukiza kuhusu chakula alichokula akiwa kituo Cha Polisi Mbowe.

Jaji: ehh Matata alijibuje shahidi kama unakumbuka?

Matata: Alisema alikula biskuti.

Jaji: Wakili muulize swali kulingana na kile alichoulizwa na upande wa mashtaka.

Matata: Mheshimiwa Jaji Sina swali jingine.

Jaji: Shahidi tunakushukuru.

Kwa sasa shahidi huyo (Ling'wenya ) ametolewa katika kizimba cha watu wanaotoa ushahidi na kupelekwa katika kizimba cha washtakiwa, ambapo ameungana wenzake


Advertisement