Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Geita wakiri kumshikilia Imam Yasin

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo akizungumzia kukamatwa kwa Imamu wa Msikiti wa GPB uliopo mtaa wa Nyankumbu mjini Geita.

Muktasari:

  • Katika taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilidaiwa Machi 13, 2024 Imamu Abdulrahmaan Yasin akiwa na mwanae akitokea msikitini kuswalisha Taraweh aliitwa na watu wawili waliofunika nyuso zao wakiwa wamevaa kiraia na kuzungumza naye na baadaye kumchukua kwa nguvu na kumuweka kwenye gari kisha kuondoka nae.

Geita. Kutokana na kusambaa taarifa mitandaoni kuwa Imamu mkuu wa Msikiti wa GPB Shell uliopo Mtaa wa Nyankumbu Mjini Geita, Abdulrahmaan Yasin ametekwa na watu wasiojulikana, Jeshi la Polisi mkoani humo limethibitisha kumshikilia.

Awali taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilidai Machi 13, 2024 imamu huyo akiwa na mwanae akitokea msikitini kuswalisha Taraweh aliitwa na watu wawili waliofunika nyuso zao wakiwa wamevaa kiraia na kuzungumza naye na baadaye kumchukua kwa nguvu.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wakati akikamatwa ulitokea mzozo baina yake na watu hao, jambo lililosababisha wafyatue risasi moja hewani na kisha wakamchukua na kumuweka kwenye gari na kuondoka naye.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 15, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa imamu huyo pamoja na watuhumiwa wengine kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu.

Kamanda Jongo amesema kutokana na tuhuma zinazomkabili na watuhumiwa wengine kutokamatwa, swala hilo lilifanywa siri na kuwa sasa ukamataji wa watuhuma wengine umekamilika.

“Kutokana na aina za tuhuma na kulikuwa na watuhumiwa wengine ambao bado tulikuwa hatujawakamata, hivyo suala la kukamatwa kwake ndio maana hatukuliweka wazi.

“Baada ya kukamilisha ukamataji wa timu nzima iliyokuwa na tuhuma tumeamua tuiweke wazi kuwa imamu huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi pamoja na watuhumiwa wengine,” amesema Kamanda.

Kamanda amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Kuhusu tuhuma zinazomkabili, Kamanda Jongo amesema anatuhumiwa kujihusisha na matukio ya kihalifu, bila kutaja aina ya tukio la uhalifu analotumiwa nao.

Kamanda Jongo amesema mkoa huo una matukio ya watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha ambayo baadhi yanasababishwa na visasi na mengine yanatokana na matukio ya uhalifu.

 “Yapo matukio ya watu zaidi ya matano, mkoa huu una changamoto ya watu kupotea kwa mazingira ya kutatanisha, wengine walipatikana, wengine bado. Wapo waliopatikana Tabora, wengine Kagera kwa kulipiza kisasi.

 “Tumefungua majalada ya uchunguzi na wengine tumewapata kama alikamatwa na vyombo vya dola tunampata,” amesema.

Ametoa mfano wa mtu aliyepotea katika mji wa Katoro na baadaye wakampa jijini Mwanza.

“Alikuwa na tuhuma na baada ya uchunguzi ndani ya vyombo alipatikana na tulijulisha familia yake,” amesema.