Polisi: Tunamshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema

Tuesday October 05 2021
chademaaapic

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashimu Issa Juma

By Bakari Kiango

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashimu Issa Juma kwa tuhuma za uchochezi wa kujenga chuki kati ya Serikali na wananchi.

Issa alikamatwa Oktoba 3,2021 mjini Unguja, Zanzibar  kisha kushikiliwa kwa muda kabla ya kusafirishwa jana Jumatatu Oktoba 4,2021 kuletwa Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.

"Uchunguzi wa shauri hili unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo," amesema Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam,Jumanne Muliro  katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Soma zaidi: Viongozi, wanachama Chadema waachiwa kwa dhamana

Juma ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba Mosi,2021 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Chadema Kinondoni.

Soma zaidi:Chadema yadai kada wake anashikiliwa na Polisi Zanzibar

Advertisement

Katika mkutano huo, Juma anadaiwa kutoa tuhumu dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, Rais mstaafu wa awamu nne,  Jakaya Kikwete, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( IGP), Simon Sirro.

Advertisement