Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi waonya waganga na tuhuma za ubakaji, ramli chonganishi

Kamishna  wa Kamisheni ya Polisi Jamii, Faustine Shilogile akizungumza wakati  akifunga mafunzo   ya kuinua ubora wa tiba asili na tiba mbadala kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala  28 kutoka  mikoa mbalimbali nchini leo Julai mosi 2023 jijini Dodoma.

Muktasari:

  • Kamishna Shilogile amesema Jeshi la Polisi litaendelea kukemea vikali waganga wanaopiga ramli chonganishi na wale wanaosema wanaouwezo wa kurudisha mali iliyopotea kwani suala hilo ni la uongo.

Dodoma. Jeshi la Polisi limewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala kujiepusha na tuhuma za vitendo vya ubakaji wagonjwa wao wenye matatizo ya uzazi kwa kudai watapata watoto kama watafanya nao mapenzi.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Julai Mosi, 2023 na Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii, Faustine Shilogile aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura, wakati akifunga mafunzo kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadalakutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Kamishna Shilogile amesema kuwa Jeshi la Polisi lina taarifa za kuwepo kwa baadhi ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala ambao sio waaminifu kwa wateja wao hasa wanawake wanaofika kwao wakiwa na matatizo ya uzazi.

Amesema baadhi yao wamekuwa wakiwabaka wanawake hao wanaofika kwao na huwaambia ili wapone ni lazima wawaingilie ili waweze kupata watoto.

“Nawaomba muepuke kufanya matukio kama vile kubaka wagonjwa wanapokuja kwenu wakiwa na matatizo ya uzazi baadhi wanapewa dawa na kuambiwa ili ifanye kazi lazima aiingiliwe na mganga,” amesema Kamishna Shilogile.

Amesema wataendelea kukemea vikali waganga wanaopiga ramli chonganishi na wale wanaosema wanao uwezo wa kurudisha mali iliyopotea kwani suala hilo ni la uongo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa tiba asili Tanzania (UWAWATA), Lucas Mlipu amesema  watendelea kutoa elimu kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala kufuata sheria na taratibu za nchi katika utoaji wa tiba.

“Sasa hivi matapeli ni wengi na kisingizio ni waganga wa tiba asili na tiba mbadala hebu Jeshi la Polisi tunaomba hili mliangalie,” amesema Mlipu.