Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi yadaka 26 wakidaiwa kufanya uharifu Tanga

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi limefungua milango kwa watu wenye ushahidi wa kutosha kwenda kutoa Mahakamani dhidi ya tuhuma zinazowakabili watu 26 walitiwa mbaroni na jeshi hilo, ikiwemo ya kuingia na kwenye Hoteli ya Mambo View iliyopo katika Kijiji cha Mambo na kufanya uhalifu.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 26 walioingia kwenye Hoteli ya Mambo View, iliyopo katika Kijiji cha Mambo, Kata ya Sunga Tarafa ya Mtae, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga na kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma za uhalifu zinazowakabili.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Leo, Novemba 09, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime imesema watuhumiwa hao walidaiwa kufanya uhalifu huo Oktoba 23, mwaka huu.

Mbali na tukio hilo, taarifa hiyo, Misime amesema watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma zingine za kufanya unyang’anyi wa kutumia nguvu na shambulio la kudhuru mwili wa ‘Dagmara Anna Ikiert’.

“Watuhumiwa hao 26, walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Oktoba 26, 2023 kujibu tuhuma hizo kwa mujibu wa sheria,”amesema

Misime amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na taasisi nyingine wanaendelea kukamilisha ukusanyaji wa ushahidi ambao unahitaji chunguzi zaidi ili kesi hiyo iweze kwenda katika hatua inayotakiwa.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mwenye ushahidi mwingine wa ukweli asisite kuufikisha polisi ili uweze kufanyiwa kazi,” amesema.

Misime amesema jeshi hilo halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote yule atakayebainika kuhusika kwa namna yeyote ile au kwa kupanga, kuhamasisha, kutoa taarifa za uongo au kufadhili,“ amesema Misime